Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe, William Tate Ole Nasha, (MB) ametoa pongezi kwa Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi , kwa kutekeleza vyema na kusimamia vizuri miradi pamoja na maendeleo ya Sekta ya Elimu Wilayani humu.
Akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri wakati wa Ziara ya kikazi Wilayani humu , Mhe, Naibu Waziri William Ole Nasha amesema kwamba amefurahishwa sana na juhudi zilzofanyika katika kutekeleza na kukamilisha miradi ya Sekta ya Elimu katika Halmashauri ya Misungwi, ikiwemo miradi ya Ujenzi wa Nyumba ya Walimu (six in one), vyumba vya Madarasa, matundu ya vyoo uliokamilika, na Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Elimu unaoendelea kwa sasa katika Halmashauri 100 nchini kote.
Mhe, William Tate Ole Nasha, Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia akizungumza kwa msisitizo kuhusu maendeleo ya Elimu kwa Watoto wa Kike ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Juma Sweda (aliyekaa kulia) wakati wa Ziara ya kikazi Wilayani humu.
Mhe, William Tate Ole Nasha, ameeleza hayo mara baada ya kupokea taarifa fupi ya maendeleo ya Wilaya iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe, Juma Sweda, taarifa iliyoonyesha mambo na shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa mwaka 2018/2019, hususani Sekta ya Elimu ambayo iliiwezesha Halmashauri kuongeza ufaulu wa Wanafunzi wa darasa la Saba kuwa Washindi wa tatu katika Mkoa wa Mwanza , sambamba na Wanafunzi wa Kidato cha Nne kuwa katika nafasi ya Nne kimkoa kati ya Halmashauri za Wilaya Nane za Mkoa wa Mwanza kwa matokeo ya mwaka 2018.
Mhe, Naibu Waziri Ole Nasha, ameridhishwa namna Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Misungwi wanavyosimamia na kutekeleza kwa kiwango na ubora miradi akitoa mfano mradi wa Nyumba ya Walimu (Six in One) katika Sekondari ya Isakamawe uliokamilika kwa gharama ya shilingi 141,000,000 na umefunguliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 ,
Amesema Halmashauri imeweza kusimamia vyema miradi ya ujenzi wa Vyumba viwili ambayo yote imekamilika katika Sekondari za Mbarika, Sanjo, Mamaye na Koromije zote kwa gharama ya shilingi 100,000,000 za ufadhili wa Serikali kuu paoja na Mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika Shule za Msingi Isela pamoja na Shule ya Msingi Sumbuka kwa shilingi 60,000,000.
Mhe, Naibu Waziri Ole Nasha, pia amewashukuru Viongozi na Watendaji Wilayani humu kwa kushirikiana katika kazi ya ujenzi walioufanya katika mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Uthibiti Ubora unaondelea ambapo wamefikia hatua ya ukamilishaji na kwa mujibu wa maelezo ya Mthibiti Ubora Mkuu wa Shule Wilaya, Faustine Salala kwamba ujenzi unasimamiwa na Kamati ya ujenzi na tayari shilingi 60,000,000 zimeshatumika kati ya fedha zote shilingi 152,000,000 zilizotolewa na Serikali kutekeleza mradi huo, na matarajio makubwa ya kukamilisha ujenzi huo mwezi Agosti mwaka huu kwa ziada ambapo fedha hiyo wameahidi kutekeleza katika kununua samani za ofisi na kuongeza miundombinu mingine muhimu.
Jengo la Ofisi ya Uthibiti Ubora Wa Elimu linaloendelea kujengwa Wilayani Misungwi,limegharimu shilingi 60,000,000 mpaka hatua ya kuweka Fremu za Milango na Madirisha, pamoja na Vigae, upigaji wa Lipu ndani na nje na Kamati ya Ujenzi inaendelea na ukamilishaji hadi mwezi Agosti mwanzoni mwaka 2019.
“ Nawapongezeni sana kwa namna mnavyoshirikiana kutekeleza na kusimamia vyema miradi na kuinua ufaulu wa Elimu katika Wilaya yenu ya Misungwi, na mumeweza kuwakamata na kuwafunga Gerezani Watu 30 wakiwemo Walimu na Watendaji wengeni waliowapa Mimba na kuwaoa Wanafunzi wa Kike”. Alieleza Naibu Waziri Ole Nasha.
Mhe, Naibu Waziri wa Elimu ameonyeshwa kukerwa na kukemea vikali mambo ya kizamani yanayofanywa na Wanachi ya kuwaoa na kuwapa Mimba Watoto wa Kike wanaosoma na kuharibu ndoto na fursa ya kuendelea kimasomo na kupoteza dira na mwelekeo wao katika maisha, na amewataka Viongozi na Watendaji wote Wilayani humu kuendelea kushirikiana na kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa Watoto kusoma ili waweze kusaidia familia zao na taifa kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.