Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza yatakiwa kuongeza kasi ya kukusanya Mapato ya Kodi ya Ardhi ili kuboresha na kuinua kiwango cha Makusanyo ya mapato nchini.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Mendeleo ya Makazi, Mhe, Angelina Mabula alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni Wilayani humo ambapo amewataka Viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanafuatilia kikamilifu Wananchi ambao hawajalipa Kodi ya Ardhi kwa muda mrefu sasa na kusababisha Serikali kukosa Mapato.
Mhe, Angelina Mabula ameagiza Menejimenti ya Halmashauri ya Misungwi kuwaandikia Kusudio la kulipa Wadaiwa Sugu wote wa Kodi ya Ardhi na kumtaka Kamishina wa Ardhi wa Kanda kufuatilia na kusimamia vizuri utekelezaji wake hata hivyo alisema atarudi tena Wilayani humo mwezi Machi 2019 na kuwaomba kutekeleza maagizo na maelekezo hayo mapema ikiwa ni pamoja na Mkakati wa Upimaji wa Viwanja kwa Wananchi ili kurasimisha Makazi.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe,Angelina Mabula akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi
Awali akitoa taarifa ya Wadaiwa Sugu wa Kodi ya Ardhi Wilayani humo Afisa Ardhi Mteule, Bi, Florida Busheni alisema kwamba takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya Shilingi 114,000,000/= ( Millioni Mia moja na Kumi na Nne tu) ni fedha za Wadaiwa Sugu ambazo ni madeni ya muda mrefu na tayari wameshawataarifu wahusika na wameandaa orodha kwa ajili ya kufikishwa Mahakamani.
Naibu Waziri Mabula, ameitaka Idara ya Ardhi na Maliasili kuhakikisha inatekeleza maelekezo ya kupima maeneo ya Ardhi ya Wananchi na kuweza kurasimisha na kuwa na Viwanja halali vya makazi, Viwanda na biashara pamoja na kutoa Hati miliki kwa Wananchi ambao wamekamilisha taratibu zote za Mipango miji na Idara ya Ardhi ihamasishe Wananchi kupima Ardhi na hatimaye waweze kuindeleza na kuwa fursa za maeneo yaliyopimwa yatakayoweza kutumika kwa Makazi na Uwekezaji wa Viwanda vikubwa na vidogo.
Madiwani pamoja na Watendaji wa Halmashauri ya Misungwi wakimsikiliza Mhe,Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula katika Ziara aliyoifanya Wilayani humo.
Amewataka pia kuanza zoezi la kuhakiki na kutambua Viwanja vyote ambavyo havijaendelezwa kwa muda mrefu na Wamiliki ama kwa kujengwa au kuendelezwa kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kupanda Miti, kinyume na hivyo Wamiliki hao wanyang’anywe Viwanja hivyo na kugawiwa kwa Wananchi wengine watakaoweza kuviendeleza kwa wakati na kulipa Kodi ya Ardhi .
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.