Serikali yapongeza juhudi za Wanawake wa Kikundi cha Witogwa kujenga Nyumba bora kumi ili kuondokana na Nyumba za Nyasi na kuwa na makazi bora katika Kata ya Usagara Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt, Godwin Mollel ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wanakikundi cha Witogwa kwenye ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi aliyoifanya hivi karibuni na kueleza kwamba Misungwi itakuwa mfano kwa Wanawake wote nchini kwa kujenga Nyumba bora ambapo Serikali itaendelea kuwapa msaada na Mikopo na kutoa ushirikiano wa karibu ili waweze kujikwamua katika maisha.
Dkt, Mollel ameshangazwa kuona akinamama wanajiunga kwenye Vikundi na kuweza kujenga Nyumba wakati maeneo mengine Nyumba bora zinajengwa na Wanaume na amefurahishwa kuona kwmba hapa Misungwi Nyumba bora sasa zinajengwa na Wanawake hivyo ni jambo zuri sana na kuwapongeza kwa jitihada na juhudi hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa Kikundi cha Witogwa, Helena Masalu amesema kwamba wanakikundi wamekuwa wakisaidiana na kuweka akiba na kujenga Nyumba ambapo hadi sasa wamejenga Nyumba 10 kati ya Wanakikundi 12 wa Kikundi cha Witogwa kilichopo Kijiji cha Idetemya Kata ya Usagara.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda amesema kwamba kutokana nan a Akinamama kujenga Nyumba bora kwa sasa Ndoa zitadumu zaidi kwa sababu Mwanaume hawezi kuvunja Ndoa na kuacha Nyumba nzuri na Familia na ataenda wapi na kuwasihi Wanawake wote Wilayani humo kuiga nakuendelea kujenga Nyumba za makazi bora.
Naye Mkurugenzi wa Shirika lisiliokuwa la kiserikali la Kivulini Mkoani Mwanza, Yssin Ally amesema kwamba wameweza kuwapa Stadi na mafunzo kwa Wanawake kujitambua na kujiamini katika maisha ya ndoa kwa kushauriana na Waume zao namna ya kupanga na kuleta maendeleo katika familia.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt, Godwin Mollel katika ziara hiyo ameweza kutembelea na kukagua maendeleo mbalimbali katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi ambapo ameweza kuona namna Chuo hicho kinavyoendesha na kuweka mipango ya kuibua vipaji vya Wataaalam katika sekta ya ufundi na kuonyeshwa mikakati ya uanzishaji wa kugundua na kutengeneza baiskeli ya Mlemavu inayotumia mfumo wa solar na namna ya kutumia pumba za Mpunga katika shughuli za ujenzi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Dkt, Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa na Wilaya na akina mama Wanakikundi cha Witogwa kilichojenga Nyumba kumi za wanakikundi cha Witogwa Kata ya Usagara wakiwa katika Nyumba ya mmoja wa Wanakikundi Salome Buzuka aliyejenga Nyumba na kukamilisha ambapo anasubiri kuunganishiwa na nishati ya umeme
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel (katikati) akicheza Wimbo wa Kisukuma pamoja Viongozi na Akina mama wa Kikundi cha Witogwa wakati akikagua na kuzungumza na Wanawake hao waliojenga Nyumba kumi kwa Wanakikundi ili kuondokana na makazi duni ya kuishi katika Nyumba za Nyasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.