Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Dkt,Faustine Ndugulile amewataka Maafisa Elimu kote nchini kuhamasisha Wanafunzi wa Sekondari wa O-level kusoma masomo ya Sayansi ili kuwa na taifa la Madaktari na Wauguzi wa kutosha katika Vituo vya kutolea huduma za Afya.
Naibu Waziri wa Afya Dkt,Ndugulile amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa kusaidia na kuimarisha utoaji wa huduma za Afya ujulikanao,"The more and better Midwives for Rural Tanzanai",unaofadhiliwa na Serikali ya Canada chini ya usimamizi wa Shirika la JPAEGO unaotekelezwa katika Halmashauri za Mikoa Nane (8) za Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi kwa kuwajengea uwezo Walimu wa Vyuo vya Uuguzi na Ukunga kuhusu uendeshaji na utoaji wa huduma za Afya kwa Wananchi.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Mradi huo ulliofanyika katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga cha Bukumbi Wilayani Misungwi,Mkoani Mwanza,Dkt,Ndugulile alisema ni wakati umefika sasa Watoto wajipange na kuhakikisha wanasoma masomo ya Sayansi kwa lengo la kuongeza na kuboresha fani ya Sekta ya Afya nchini kwa kutoa huduma bora za Afya kwenye Vituo vyote vya Afya kupitia Wataalamu wa Afya na kuweza kupunguza changamoto ya Vifo vya Akina mama Wajawazito na Watoto.
Alieleza kuwa changamoto ya Vifo vya Akina mama Wajawazito na Watoto ipo ambayo inakadiriwa kwamba kati ya Akinamama wajawazito 100,000 ambapo kunatokea Vifo takribani 556 ambavyo husababishwa na baadhi yao kutojifungulia katika Vituo vya kutolea huduma za Afya na kutozingatia kanuni na Miongozo ya Afya
Naibu Waziri wa Afya Dkt,Ndugulile alibainisha matarajio na na mipango ya Serikali katika kuboresha huduma za Afya nchini ambapo inatarajia kuajiri Watumishi wa Sekta ya Afya wapatao 3,410 hivi karibuni mara baada ya taratibu za kabali cha ajira kukamilika, ili kuwezesha kuimarika na kuboresha huduma za Afya kwenye maeneo ya Zahanati,Vituo vya Afya an Hospitali za Wialya na Mikoa.
Amesema katika jitihada ambazo Serikali inaendelea kuchukua za kuboresha na kuimarisha Sekta ya Afya nchini kwa kushirikiana na Wadau na Wahisani mbalimbali wa Maendeleo ni pamoja na kutoa Magari ya Wagonjwa (Ambullance) zaidi ya 50 zilizotolewa na kugawiwa hivi karibuni katika Wilaya na Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupunguza changamoto ya Vifo vya akina mama Wajawazito na Watoto.
Ametoa wito kwa Wananchi wote kuthamini na kutambua umuhimu wa huduma za Afya zitolewazo na kuwaomba kuhudhuria katika Vituo vya kutolea huduma za Afya kwa ajili ya kupima Afya zao na kupata matibabu sahihi kwa wakati muafaka na kuwataka kutojihusisha na vitendo vya utoaji wa Rushwa kwa lengo la kupata huduma za Afya.
Awali akizungumza na Wananchi na akitao Salamu za Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda,aliwashukuru Wadau wote wa Maendeleo hususan wa mradi huo ana kuahidi kusimamia kikamilifu ili uweze kuleta tiaj na ufanisi kwa manufaa ya Wananchi wa Misungwi na taifa na kuwataka Wauguzi na Wakunga wote kuchapa kazi kwa kutoa huduma bora za Afya kwa kuzingatia miongozo na kanuni na maaadili ya fani ya Sekta ya Afya na kuleta matokeo chanya .
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito kwa Wananchi wilayani humu kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya kwa kila kaya kuchangia Tsh,10,000 kwa ajili ya kuwezeshwa kupewa matibabu kw awatu 6 toka kwenye Familia ambapo takwimu zinaonyesha kwamba hadi sasa ni wananchi takribani 9,100 tu ndio wameshajiunga kwenye mfuko wa bima ya afya wilayani na kwa upande wa utoaji wa huduma zaAfya kwa Wazee tayari Halmashauri imeshawapatia Vitambulisho zaidi ya Wazee 12,000 na zoezi linaendelea kwa wilaya nzima.
.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.