Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe,Mwanaidi Ally Khamis awataka Watumishi kutumia taaluma zao kusaidia Watoto hasa wa kike na Taifa kwa ujumla Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa jana wakati wa ziara ya Naibu Waziri Maendeleo Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Mhe,Mwanaidi Khamisi alipotembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Ujenzi wa mabweni katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi ambapo amewataka Watumishi kutumia taaluma zao kusaidia makundi maalumu wakiwemo,Wazee na Vikundi vya akina Mama ili kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo wanakoishi.
“Napenda kuwasihi Watumishi wote kutumia taaluma zao kuwasaidia na kulisaidia Taifa ili kuhakikisha wataalamu wenye fani mbalimbali za Maendeleo ya Jamii kutoa elimu kwa jamii nzima. “
Aidha Naibu Waziri Mhe,Mwanaidi Khamis amesisitiza kuwa Serikali imetoa Fedha za kutosha kwa ajili ya kukamilisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita na kutoa wito kwa wakandarasi kusimamiwa kikamilifu ili kufanya kazi zao kwa wakati.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha amesema kumekuwa na vitendo vya Watoto kike kuodheshwa wakiwa na umri mdogo jambo ambalo halikubaliki na Serikali imekuwa ikipambana na vitendo hivyo viovu ili kuvikomesha visitokee tena na kuwaonya watu wenye nidhamu mbaya kuacha kwa hiari vitendo hivyo na wasithubutu kuoa Watoto wadogo wala kuwafanyia unyanyasaji wa aina yeyote ile ikwemo kuwakatisha masomo ili waolewe.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Misungwi Bi,Ester Msoka ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Misungwi hapo awali akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa Ofisi ya Maendeleo Jamii imekuwa na uhaba wa watumishi katika fani hiyo pamoja na ukosefu wa vyombo vya usafiri wa kwenda maeneo ya kazi na kuomba kupatiwa gari pamoja pikipiki ili kurahisisha usafiri na utoaji wa elimu kwa Wananchi kwa wakati.
Naye Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi {CDTTI} Bw, Charles Achuodho amesema kuwa Ujenzi wa mradi utakapokamilika utagharimu Shilingi Bilioni 2.2 ambapo awamu ya kwanza wamepewa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 300.Pia ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambayo inafanyika katika chuo hicho.
Diwani wa Kata ya Bulemeji Mhe,Rahma Fedelis ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kutoa fedha zaidi ya shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari Bulemeji na Wananchi hawakuchangishwa fedha katika ujenzi huo wa madarasa lakini pia Mradi wa Maji wa Kata ya Bulemeji ambao bado unaendelea kutekelezwa kwa ajili ya manufaa ya Wananchi wa kata hiyo.
Naibu Waziri Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe,Mwanaidi Ally Khamis akisikiliza taarifa kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi Bw,Charles Achuodho jana mapema katika ziara yake ya kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo chuoni hapo.
Naibu Waziri Bi Mwanaidi Khamis akiwa katika picha ya pamoja na Wazee wa Kituo cha Kaluande Bukumbi ambapo alitembelea na kuona makazi yao na kuwashili Viongozi waendelee kuwatunza na kuwalea vyema.
Naibu Waziri Mhe,Mwanaidi Khamis akisalimiana na Viongozi wa Ngazi ya Wilaya ya Misungwi hapo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua shughuli za miradi ya Kijamii Wilayani Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.