Naibu Waziri Mhe,Patros Katambi atoa siku 7 kwa Mkandarasi Chuo cha Uhasibu TAA Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Patros Paschal Katambi ametoa siku 7 kwa mkandarasi kutatua changamoto za wafanyakazi wa katika ujenzi wa mradi wa Chuo cha Uhasibu kilichopo kijiji cha Nyang’omango kata ya Usagara ambapo alimtaka mkandarasi CRJE kuhakikisha anatatua changamoto zinazowakibili wafanyakazi wa Chuo hicho ikiwa pamoja na kunyanyaswa kwa wafanyakazi na kucheleweshewa maslahi yao.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri alipotembelea mradi wa Chuo hicho cha Uhasibu wakati akisikiliza kero za changamoto zinazowakabili wafanyakazi ambapo amesema haikubaliki kuona wafanyakazi wananyanyaswa na kucheleweshewa au kutolipwa stahiki zao kwa wakati na hata mfumbia macho mtu yeyote atakaye kiuka maelekezo aliyoyatoa.
“Tusiwatumie hawa watu kama punda hawa ni bindamu na mnawaona ni vijana majabali kabisa ni wazuri kwa ajili ya nguvu kazi ya Taifa “
Katika ziara hiyo Mhe,Naibu Waziri Kazi,vijana,Ajira na Wenye ulemavu Mhe,Katambi amesema chuo hicho kimekamilika kwa asilimia 45 na mkandarasi ameshalipwa kiasi cha bilioni 1.6 ambapo amesema mradi huo ni chachu kubwa kwa ustawi wa ajira ,vijana na kazi ndani ya mkoa wa Mwanza,taifa na ulimwengu kwa ujumla.
Kwa upande wake Afisa kazi mfawidhi Bi, Betty Mtega katika mradi wa chuo cha Uhasibu amesema kuwa hapo awali hapakuwa na mahusiano mazuri kati mkandarasi na Wafanyakazi ambapo wafanyakazi waligoma kusaini mikataba kwa sababu hawajui mwajiri wao ni nani,hata hivyo Bi,Betty amsema suala hilo limefanyiwa kazi na wafanyazi wamepewa mikataba pamoja na kulipwa mishahara kwa mujibu wa sheria.
Kwa nyakati tofauti Mhe,Naibu Waziri pia alitembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la JP Magufuli lenye urefu wa kilomita 3.2 ambapo amesema ujenzi wa daraja hilo utachukua nafasi ya vivuko na kuwa kiungo muhimu kati ya mkoa wa Mwanza na nchi jirani za Rwanda ,Burundi na Uganda utasaidia kupunguza msongamano wa magari kwenye kivuko,utapunguza muda wa usafiri na kuboresha usafiri kwa umma.
Aidha amesema kuna haja ya kuwatambua vijana kwa uzalendo wao wa kufanya kazi katika miradi mbalimbali hapa nchini kwa kupelekwa vyuo ili wapate ujuzi zaidi na kupewa vyeti ikiwa pamoja na kuingizwa kwenye kanzidata ili watambulike na inapotea miradi mingine wapewe kipaumbele.
Sambamba hilo ameonya vijana wenye tabia ya wizi na udokozi kuacha mara moja kwani kufanya hivyo watafukuzwa kazi na hivyo kukosa kipato. Badala yake wawe mabalozi wazuri na washirikiane kwa pamoja katika kufanya kazi ili kuijenga nchi yao.
Meneja NSSF mkoa wa mwanza Bw,Emmanuel Kahensa amesema kuwa ameyachukua maelekezo ya Naibu Waziri na kwamba atayafanyikia kazi ikiwemo kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati na kufanyia kazi changamoto ambazo zimejitokeza wakati wa kazi.
Naye Rajabu Seleman mkazi wa nyang'omango amesema kwa niaba ya wafanyakazi wenzake ameshukuru ujio wa Naibu Waziri kwa kuja kusikiliza kero na changamoto na kupatiwa ufumbuzi,ziara hiyo imewapa imani kubwa kuwa Serikali ya awamu ya sita iko kazini,na ameahidi kuwa watafanya kazi kwa bidii.
Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu mhe,Patros Katambi kushoto na kulia ni katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw, Petro Sabato wakiongozana na mweji wa ziara hiyo katika ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa daraja la JP Magufuli hapo jana ambapo amekagua na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Mwonekano wa jengo la Chuo cha Uhasibu TAA ,kata ya Usagara kijiji cha nyang'omango ambapo Mradi huu umefikia asilimia 45 mpaka sasa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu TAA wakisikiliza kwa makini na kutoa changamoto zao katika ziara ya ukaguzi wa miradi na Naibu Waziri Mhe,Patros Katambi hapo jana.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.