Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Christina Mndeme asifu na kupongeza ujenzi wa Shule ya Sekondari ya bweni ya wasichana Mwanangwa Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Bi. Christina Mndeme ametoa pongezi hizo katika ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na kupongeza serikali na Wananchi kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwanangwa katika Kata ya Mabuki itakayokuwa na wanafunzi 160, na bweni la wasichana pamoja na maabara.
Aidha amesema kuwa eneo la ujenzi wa Mradi wa shule ya Sekondari hiyo lipimwe na kuwekwe mipaka liwe hati miliki ili kuondoa migogoro ambayo inaweza kujitokeza,Sambasamba na hilo amesisitiza kuwepo na miundo mbinu ya maji,umeme na ulinzi wa kutosha ili kuwalinda wanafunzi na walimu wasivamiwe.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Veronika Kessy amsema kuwa ujenzi wa Shule hiyo utakapokamilika utaondoa adha kwa wanafunzi wa kike ya kutembea umbali mrefu Zaidi ya kilomita 6,hivyo itatatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kike kutembea umbali mrefu na kuwapa hamasa ya kubwa ya kujisomea.
Akitoa taaarifa kwa niaba ya kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi. Bi ,Gloria Bunane alieleza kwamba shule hiyo itagharimu Zaidi shilingi milioni 700,000,000/=ambapo ujenzi wa Shule hiyo utakuwa awamu mbili ,awamu ya kwanza itaanza na majengo 4 ambayo yatagharimu shilingi milioni 457,000,000/= likiwemo bweni moja la wasichana ,bwalo kwa ajili ya chakula na vyumba vya madarasa 4 , ofisi ya walimu pamoja na jengo la maabara lenye vyumba viwili.
Bi,Gloria Bunane amesema kuwa ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana unatarajiwa kukumilika mwezi januari 2023 na shule hiyo itapokea wanafunzi wa kike kutoka sehemu mbalimbali ya Wilaya ya Misungwi .
Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Ndg, Christina Mndeme kushoto akisalimiana Viongozi wa mbalimbali wa ngazi ya Misungwi wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Mhe,Rahma Fidelis akifuatiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Mhe, Kashinje Machibya mara baada ya kuwasili katika Mradi wa Ujenzi wa Sekondari ya Mwanangwa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Ndg,Christina Mndeme akishiriki kwa vitendo katika Ujenzi wa ukuta wa jengo la bweni la wasichana Sekondari Mwanangwa Wilayani Misungwi
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.