Vijana wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza waaswa kuzalisha mali kwa wingi ili kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Akitoa wito huo mapema leo Kiongozi wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josphine Paulo Mwambashi wakati wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2021 zilizokimbizwa na kukagua, kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi tisa ya Wilaya ya Misungwi.yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.5.
Luteni Mwambashi amesema vijana wanapaswa kutumia fursa zilizopo na kuongeza bidii katika kazi na kuzingatia maadili ya na ueledi mkubwa pamoja na kujifunza sambamba na kuwajibika kikamilifu katika kujleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Amewataka Watanzania kuchukua tahadhari zote kwa kujikinga na maambukizi mapya ya COVID 19, rushwa na madawa ya kulevya, maabukizi ya virusi vya Ukimwi na ukimwi pamoja na ugonjwa wa Malaria kwa lengo la kujenga taifa imara na lenye afya njema kwa Wananchi.
“ Nawaomba Wananchi mjiepushe na rushwa na muweze kuipinga vikali kwa sababu ni adui wa haki na hurudisha nyuma maendeleo endapo ikiendekezwa na kufumbiwa macho”. Ameseama Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa msisitizo.
Amewataka pia kuzingatia matumizi bora na sahihi ya vifaa vya TEHAMA kutokana na kuwa na mchango mkubwa katika shughuli zote za uzalishaji na kukuza uchmiikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya kielektroniki na mtandao sambamba na kukuza biashara.
Awali akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ufugaji wa kuku katika Kijiji cha Idetemya wenye tahamani ya milioni 500 alisema amefurahishwa na kuvutiwa nan a kitendo cha Mwekezaji wa kizalendo na kuwa na imani kubwa kwamba uwekezaji huo utaleta tija kwa Wananchi kupata fursa za ajira hususan vijana waliop eneo la Wilaya ya Misungwi ikiwemo na kuchangia mapato ya Serikali kuu na hatimaye kuchochea maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Veronica Kessy amesema mbio hizo za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Misungwi zimefanikiwa kuzindua, kukagua na kuweka jiwe la msingi katika miradi tisa ikiwemo mradi wa shughuli za kikundi cha Uvuvi, Mradi wa darasa la Komputer, mradi wa ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji, mradi wa ufugaji wa kuku, mradi wa usafiri wa Bajaji kwa Mlemavu, mradi wa maabara ya Sayansi, mradi wa ujenzi wa barabara ya Lami, mradi wa shughuli za utafiti wa Malaria pamoja na mradi wa ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Misungwi.
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Paul Mwambashi, akizindua Jengo la Wodi ya wazazi katika Hospitali ya Misungwi Mapema hii leo
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronica Kessy, akishika Mwenge wa Uhuru wakati wa risala ya utii kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru Wilayani Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.