Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 umefungua na kuweka Jiwe la Msingi katika Miradi sita yenye thamani ya shilingi Bilioni 1,212,349,130/= kati ya Miradi saba yenye jumla ya shilingi Bilioni 1,638,287,062/= ulipokuwa unakimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza mapema jana.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Mzee Mkongea Ali aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa kutekeleza Miradi vizuri na kwa ubora na kwa kuzingatia viwango vya ujenzi vinavyotakiwa chini ya usimamizi wa Viongozi wote pamoja na Mhandisi wa Ujenzi na kuhakikisha inatekelezwa na kukamilika kwa wakati na kufuata vipimo na maelekezo ya Serikali ya awamu ya tano.
Jengo la Bima ya Afya lilojengwa katika Hospitali ya Misungwi
Mzee Mkongea Ali alitoa pongezi hizo wakati akizindua na kufungua Mradi wa Nyumba ya Walimu Six in One katika Sekondari ya Isakamawe wenye thamani ya shilingi Milioni 141,000,000/= pamoja na Mradi wa Jengo la Bima ya Afya Katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi uliotekelezwa kwa shilingi Milioni 198,028,930/=, miradi ambayo imejengwa kwa ubora na kiwango na kulingana na thamani ya fedha iliyotumika na amewataka Wananchi wayatumie na kuyatunza Majengo hayo vizuri ili yaweze kutoa huduma kikamilifu sambamba na kudumu kwa muda mrefu.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Peter Michael akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Joseph Kapunda tarehe 15 Mei mwaka huu.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wakati akitoa ujumbe wa Mwenge kwa mwaka 2019, amewataka Wananchi wa Wilaya ya Misungwi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi Oktoba mwaka 2019 ili kuweza kutumia haki ya kikatiba ya kuchagua Kiongozi anayemtaka kwa kuzingatia sifa na vigezo, pamoja na kuongeza bidii katika kuchapa kazi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Mhe,Rais wa Tanzania katika kujenga uchumi wa kati na wenye Viwanda vingi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda awali akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kisena Mabuba ambaye awali alikabadhiwa Mwenge huo wa Uhuru na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio, alisema kwamba Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Misungwi zitakimbizwa kwa umbali wa kilomita 115 na kufungua, kuweka jiwe la Msingi, kuzindua na kukagua jumla ya Miradi 7 yenye thamani ya Bilioni 1,638,287,062/= ambayo ni miradi ya Sekta ya Viwanda, Maji, Elimu, Barabara, Afya, na Mazingira ambapo Kauli Mbiu ya mwaka huu 2019 ni Maji ni Haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na Tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu, Wilayani Misungwi umepokelewa Kimkoa katika Kijiji cha Mwawile, Kata ya Nhundulu, kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Mkoa wa Shinyanga na Wilaya ya Misungwi ilikabidhi Mwenge huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema tarehe 15, Mei 2019.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.