Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yapokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 na kuukimbizwa na kuzindua Miradi, kuweka jiwe la Msingi, kukagua na kufungua miradi ya Maendeleo minane (8) yenye jumla ya gharama ya Shilingi 2,381,277,750/= .
Akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Bujingwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Juma Sweda alieleza kwamba Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambapo utakimbizwa katika maeneo mbalimbali katika Wilaya kwa umbali wa kilomita 108.7.
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi umekimbizwa katika Mradi wa Kiwanda cha Gesi ya Majumbani cha Usagara chenye gharama ya Shilingi 790,000,000, ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Francis Kabeho amewataka wananchi kutumia Gas ili kuweza kulinda raslimali za Misitu na kuachana na matumizi ya Mkaa na inarahisisha kazi ya mapishi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Charles Francis Kabeho amefungua mradi wa mtandao wa barabara ya Misungwi mjini yenye Shilingi 42,682,500, na kuwataka Wahandisi kuzingatia kanuni na taratibu katika usimamizi wa matengenezo ya barabara pamoja na kuzindua Mradi wa Bwawa la Samaki Sawenge wenye Shilingi 154,700,000.
Miradi mingine iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na Mradi wa uhifadhi wa Maji na kisima Mitindo wenye Shilingi 68,797,000/= Mradi wa ujenzi wa Jengo la Kitengo cha Bima ya Afya Hospitali ya wilaya lenye thamani ya Shilingi 141,525,250, Mradi wa Shule ya Sekondari ELPAS kwa gharama ya Shilingi 1,020,000,000, Shughuli ya Utoaji wa Mikopo kwa Vijana, Wanawake na Walemavu Shilingi 50,000,000 na Mradi wa Maabara ya Kompyuta wa Mitindo wenye gharama ya Shilingi 113,573,000. Aidha, fedha hizo zinatokana na mchango wa Halmashauri ambazo ni shilingi 196,625,250, mchango wa Serikali kuu kiasi cha shilingi 106,282,500 pamoja na fedha za michango ya Wahisani kiasi cha shilingi 2,078,370,000/=
Mmoja wa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa akifurahia na Watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi maalum ya Mitindo
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika maeneo ya miradi amesisitiza kuhusu ujumbe Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 ambao ni ‘’Elimu ni ufunguo wa maisha Wekeza sasa kwa maendeleo ya taifa letu” na amewataka Wananchi wote wa Wilaya ya Misungwi kupeleka watoto shule hususan katika kipindi hiki cha elimu bure na Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuhudumia elimu nchini hivyo ni vyema wakawasimamia watoto wasome vizuri kwa manufaa ya taifa kwa ujumla..
Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema siku ya Jumatano tarehe 29/08/2018 katika Kijiji cha Busisi na kukimbizwa katika Halmashauri ya Sengerema na Buchosa Wilayani Sengerema.
KIongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg,Charles Francis Kabeho (Katikati) akikata Utepe kwenye mradi wa mabwawa ya Ufugaji wa Samaki Sawenge akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Juma Sweda,Diwani wa Kata ya Igokelo pamoja na Wamiliki wa Mradi huo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.