Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendeji wa Halmashauri, Mweka Hazina wa Halmashauri, Bwana Itendele Maduhu akitoa maelekezo kuhusu kodi ya majengo ambayo ilianza kutozwa mapema Mei, 2017 baada ya kukamilika kwa sheria ndogo ya kodi hiyo, kodi ya majengo ni miongoni mwa vyanzo vya mapato vya Halmashauri.
Sambamba na hilo, Mhasibu wa Mapato, Bwana Dotto Hosea aliwasilisha maada juu ya ulipaji kodi ya majengo kwa uongozi wa kata ya Misasi, vilevile aliwaagiza watendaji wa vijiji kwenda kuwahamasisha wananchi ili waweze kulipa kodi kwa wakati. Kwa mara nyingine, Mweka Hazina aliwasisitiza Watendaji wa vijiji kuzingatia vigezo vya ulipaji kodi ili kuepuka kero kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.