Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza, yakabidhi Bajaji ya abiria yenye thamani ya Milioni 7. 8 kwa Mwanamke mwenye ulemavu wa miguu Mkazi wa Kijiji cha Nyangh’omango Kata ya Usagara.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe, Juma Sweda amekabidhi Bajaji ya abiria kwa Yunis Joshua mwanamke mwenye ulemavu ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyangh’omango Kata ya Usagara Wilayani Misungwi na kuitaka jamii kuendelea kuwajali na kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waweze kujikwamua na kujikomboa na maisha na kukuza uchumi binafsi na familia zao.
Amesema Serikali inathamini uwepo wa watu wenye ulemavu na tayari Halmashauri imetiza wajibu wake kwa kutoa mkopo na ameitaka jamii na Wananchi kwa ujumla kuwaibua watu wenye ulemavu walioko majumbani
Amemtaka mama huyo mwenye ulemavu kuendelea kupambana na maisha kwa kutumia chombo alichopewa kujikwamua kimaisha na kumsaidia sana hatimaye kuondoa kudharaulika kwa jamii.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Bajaji mama huyo mwenye ulemavu Bi. Yunis Joshua ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa namna inavyowajali na kuweza kuwapatia mikopo kutokana na jamii kutowatambua na kwamba wao ni wakusaidiwa na kubebwa mara kwa mara tu na hawawezi kufanya lolote.
Amesema Serikali imewatambua na kuwathamini watu wenye ulemavu na kuahidi kwamba chombo hicho ataenda kukitumia kikamilifu katika kuzalisha mali na kujikwamua kimaisha na kiuchumi na kujikomboa katika maendeleo na kuwa katika hali nzuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi. Kisena Mabuba amesema kwamba Halmashauri imeamua kumpatia mkopo huo kutokana na watu wengine wenye ulemavu kutopatikana ambapo mkopo huo unatokana na asilimia 2% za watu wenye ulemavu, na mkopo huo umetolewa kwake binafsi tofauti na utaratibu wa kawaida wa kujiunga kwenye kikundi.
Ameeleza kuwa Halmashauri ina imani kwamba mama huyo atafanya biashara ya usafiri wa bajaji na atapata kipato na ataweza kurejesha mkopo huo kwa wakati ili watu wengine pia waweze kukopa na kunufaika.
Halmashauri hiyo hadi mwezi Disemba mwaka wa fedha 2020/2021 imetoa mikopo yenye thamani ya milioni 30,055,000/= kwa vikundi vinne vya watu wenye ulemavu vya Walemavu Misasi Tujijali, mkopo wa Milioni 8,000,000/= Fursa Tunaweza milioni 6,210,000 na Kikundi cha Walemavu cha Imani Chawata mkopo wa Milioni 8,000,000/= pamoja na mkopo wa milioni 7.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda akimkabidhi Bajaji na kumpongeza Bi,Yunis Joshua mtu mwenye ulemavu aliyopewa kama Mkopo na Halmashauri kwa ajili ya kujikwamua katika maisha
Bi. Yunis Joshua Mwanamke mwenye Ulemavu wa Miguu akiwa katika chombo cha Usafiriaina ya Bajaji chenye thamani ya Milioni 7.8 mara baada ya kukabidhiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ikiwa ni Mkopo kwa Watu wenye Ulemavu wa asilimia 2% ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.