Mvua ya upepo yaezua vyumba vya Madarasa na Nyumba za Walimu Shule ya Sekondari Aimee Milembe na Shule ya Msingi Isuka na kusababisha hasara zaidi ya Shillingi Millioni 15 zinazohitajika ili kurejesha Miundombinu ya Majengo hayo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari walipotembelea maeneo yaliyoathirika Afisa Elimu Sekondari Wilaya Bi,Dianah Kuboja alisema kwamba Mvua iliyoambatana na upepo imesababisha kuezuliwa kwa vyumba vya Madarasa 4, Majengo mawili ya Maabara na vyoo vya Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe pamoja na vyumba viwili vya Madarasa na choo cha Wanafunzi katika Shule ya Msingi Isuka Kata ya Kasololo,vilivile upepo huo uliezua Nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Msingi Kwimwa.
Jengo la vyumba 2 vya Maabara vilivyoezuliwa na Mvua ya upepo katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe..
Bi, Dianah Kuboja alieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya inaendelea na kufanya tathmini kupitia Timu ya Maafa ili kupata takwimu halisi za uharibifu wa miundombinu uliotokea na kuweza kuweka mikakati ya madhubuti ya kurejesha haraka iwezekanavyo ambapo tathmini ya awali imeonyesha kwamba zinatakiwa zaidfi ya Shillingi Millioni 15 kwa ajili vifaa vya kukarabati na kuezeka majengo yaliezuliwa na hatua za kuwashirikisha Wananchi zinaendelea pamoja na kufanyika kwa harambee iliyowezesha kupatikana shillingi 800,000/= katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe.
Ametoa wito kwa Wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza ili waweze kutoa msaada wa hali na mali na kunusuru maafa hayo na kuwezesha miundombinu hiyo kukamilika kwa wakati na wanafunzi pamoja na Walimu waweze kuendelee na masomo kama kawaida.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Mhe,Juma Sweda alieleza kwa masikitiko kuhusu Maafa yaliyotokea na kusababisha kuezuliwa kwa miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari ambapo Madarasa na vyoo vimeezuliwa na kusababisha kero kwa Wananchi na Wanafunzi,amesema Wilaya imeweka mikakati ya kurejesha miundombinu kwa haraka baada ya kupata tathmini ya uharibifu ya miundombinu iliyoezuliwa na amewataka Viongozi wa Kata na Vijiji kuweka utaratibu wa kurudishia baadhi ya miundombinu midogo midogo ya vyoo na Halmashauri pamoja na Wadau wengine kuweza kurejesha miundombinu ya majengo ya mapema.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Mhe,Juma Sweda (Kulia) akisimamia zoezi la Harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Maafa ya Mvua ya upepo katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe. (Kushoto) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi,Mhe,Antony Bahebe Masele akishuhudia namna Wananchi wanavyojitolea kuchan
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.