Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama ametoa rai kwa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata na Kijiji kuzingatia maelekezo yaliyotolewa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 ikiwemo kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kuwezesha Uchaguzi wa haki na huru kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Bw. Missama ameyasema hayo tarehe 30 Septemba wakati wa ufunguzi wa Semina ya Uchaguzi ya kuwawezesha Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata na Kijiji uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ameleza umuhimu wa Semina kuwa ni jambo la msingi ili kuwapa elimu na kufahamu taratibu za Uchaguzi na kuhakikisha kuwa Uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, huru na haki ambapo Semina hiyo ni muhimu kwa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata na kijiji pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo na kujadili changamoto zinazoweza kutokea na jinsi ya kuzitatua kwa njia ya kitaalamu kulingana na mafunzo hayo.
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw, Dickson Kawovela amesema kwamba Washiriki wa Semina wanatakiwa kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao, kutoa maelekezo kikamilifu kwa kila hatua ya uchaguzi pamoja na kuhamasisha jamii kujiandikisha na kupiga kura, na kuhifadhi usalama wa uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa na Waziri mwenye dhamana ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI ili kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za mitaa unakuwa wa haki na uwazi kwa faida ya Wananchi na taifa kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.