Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza Mhe,Juma Sweda apasha Mazoezi ya Viungo pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ikiwa ni kujenga mwili na kulinda Afya kwa kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Mkuu wa Wilaya huyo aliagiza Watumishi wote wa Idara na Vitengo vyote vya Halmashauri pamoja Watumishi wengine wa taasis zingine za Umma zilizopo katika Wilaya hiyo kufanya mazoezi angalau moja kwa kila mwezikwa ajili ya kulinda na kutunza Afya zao.
Akiwa katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwa kukimbia umbali wa takribani kilomita 2.5 kutoka katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Misungwi hadi Uwanja wa Shule ya Msingi Misungwi Mhe,Juma Sweda amewapongeza na kuwashukuru Watumishi wote waliojitokeza kufanya mazoezi na kueleza kuwa ni vyema kila Mtumishi na Mwananchi wa kawaida kujiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweza kujiepusha na kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo Kisukari,Moyo na mengine.
Amewataka Watumishi kuendelea na tabia ya kupenda kufanya mazoezi ili iwe kawaida na kujenga moyo wa kuwajibika katika majukumu yao ipasavyo kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa Wananchi na jamii yote.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.