Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ameagiza kuundwa kwa Baraza la Wazee la Wilaya ili kutoa fursa kwa Wazee wote wilayani humu kuwa na Chombo kinachoweza kujadili masuala na changamoto zinazowakabili ikiwemo mambo ya upatikanaji wa huduma za Afya,masuala ya Ulinzi na Usalama pamoja ukatili na unyanyapaa unaotokea miongoni mwa jamii ya Watanzania.
Mkuu wa Wilaya,Juma Sweda aliyasema hayo wakati akiwahutubia mamia ya Wananchi walishiriki katika maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wazee Duniani iliyofanyika Kiwilaya katika Kata na Kijiji cha Koromije kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Koromije,ambapo alieleza kuhusu kuundwa kwa Baraza la Wazee la Wilaya ambalo litaundwa hivi karibuni kutokana na Wenyeviti wa mabaraza ya Wazee ya Kata yaliyokwisha kuundwa kwenye Kata zote 27 ili kuweza kuwa na chombo kinachowasemea Wazee wote Wilayani kwenye masuala na mambo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Alieleza na kubainisha changamoto ziinazowakabili Wazee ambazo ni pamoja na Ukatili ,Unyanyasaji, Vitisho na Mauaji ya Wazee kutokana na utofauti na umbali uliopo kati ya Wazee na Vijana kwenye jamii ambapo Vijana wengi wamekuwa na tamaa na kuwa na fikra mbaya na mawazo ya kupata mali na Ardhi ya Wazee na hatimaye kutowathamini na kuamua kuwanyanyasa,kuwapa Vitisho na mara nyingine kusababisha Mauaji kwa Wazee alitoa wito wa kuendelea kutoa Elimu kuhusu amani na upendo miongoni mwa jamii ili kuondokana na matatizo.haya.
Aliwataka Viongozi na Watendaji wa Kata na Vijiji kutoa elimu na kufuatilia na kusimamia kikamilifu masuala yanayowakabili Wazee ikiwemo masuala ya upatikanaji wa huduma za Afya na kuhakikisha Wazee wote wanapata matibabu bure na kupewa kitambulisho maalum kinachomtambulisha Mzee kuachana na masuala ya imani potofu zinazosababisha mauaji kwa Wazee,hivyo Viongozi wote wa Vijiji kuhimiza Wananchi kutoa taarifa za Siri kuhusu mambo yanayoendelea Vijijini yanayokiuka maadili na mienendo ya Watanzania yanayoleta hofu na kukosekana kwa amani kwa Wazee na kueleza kwamba Serikali .itazifanyia kazi taarifa hizo na kuchukua hatua.
Juma Sweda,aliwataka pia Watendaji Vijiji wakishiriana na Waganga Wafawidhi kuhakikisha wanaanzisha na kuboresha huduma za Afya kwa kuanzisha Madirisha ya Matibabu kwa Wazee kwenye Zahanati na Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vilivyoko kwenye wilaya ya Misungwi ili kurahisisha utoaji huduma kwa Wazee hao.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.