Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija apongeza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Misungwi kwa usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato ya ndani kuishia mwezi Disemba 2024 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Misungwi Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na amewataka kuhakikisha wanafikia malengo yaliodhimiwa katika kukusanya mapato ya ndani kwa kukusanya shilingi Bilioni 4.7 hadi kufikia Juni 2025 na kuwataka kuongeza ushirikiano wa dhati baina ya Madiwani na Wataalam ili fedha zisimamiwe vizuri pamoja na miradi iliyopo na iweze kuleta maendeleo huku akisisitiza kuwa Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Taasisi za umma, Viongozi na Wataalam wote kuhakikisha wanasimamia vizuri makusanyo ya ndani na Miradi ya maendeleo kwa umakini mkubwa ili kuwaletea maendeleo Wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Mhe. Kashinje Machibya ameeleza kwamba katika kufikia malengo ya maendeleo ushirikiano wa dhati baina ya Madiwani na Wataalam umekuwa sehemu ya kufanikiwa kwa ukusanyaji wa mapato ya ndanipamojsa na miradi ya maendeleo kuishia mwezi Disemba mwaka 2023/2024 kuhakikisha kuwa wanafuata agizo la Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba Halmashauri zote nchini zikusanye mapato ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya Wananchi.
Vile vile Mhe, Machibya ameeleza kuwa kuwepo kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani inaashiria kuwa watendaji wanakusanya vyema na ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ikiwemo vituo vya Afya pamoja na ujenzi wa madarasa na miondombinu ya umeme
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi Bw. Addo Missama amesema kwamba Menejimenti kwa kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji wataendelea kukusanya mapato kwa bidii ili kufikia malengo waliojiwekea katika Halmashauri ili kuendelea kutatua changamoto za Wananchi kwa kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuhakikisha kuwa sekta za afya, Elimu , Miondombinu ya Barabara, umeme, maji, kilimo na uvuvi Viwanda na Biashara vinaimarika kwa huduma bora.
Wakati huo huo, Diwani wa Kata ya Misasi Mhe, Daniel Busalu na Mtendaji wa Kata ya Bulemeji Bw. Habbibu Amir wameishukuru Serikali ya awamu sita kwa kuendelea kuleta fedha za miradi hususani sekta ya Elimu pamoja na miradi ya sekta ya maji inayotekelezwa ushirikiano na mshikamano ambao wanautoa katika kuhakikisha wanasimamia vizuri makusanyo mapato ya ndani ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kutoa rai kwa taasisi ya TARURA,TANESCO,RUWASA kuchukua hatua madhubuti za kuwatumikia Wananchi katika kutatua changamoto walizo nazo kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.