Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe, Adam Malima ahimiza Halmashauri kuongeza ukusanyaji wa Mapato Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Adam Malima katika ziara ya kujitambulisha na kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi Wilayani Misungwi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 kwa kuvuka asilimia mia moja.
Amesema hayo katika ukumbi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi ambapo ametoa dira ya maendeleo katika kuwahudumia Wananchi kufuatia kuteuliwa hivi karibuni na Mhe,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kuongoza Mkoa wa Mwanza.
“Napenda kuwapongeza sana Mkurugenzi na timu ya menejimenti yako kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani mmevuka malengo yenu lakini pamoja hilo muongezee ubunifu na jitihada za dhati katika kukusanya mapato ili kufanikisha malengo mliojiwekea ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.1 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.” Alisema Mhe, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza na Watumishi Wilayani Misungwi ametoa rai kwa Mamlaka ya MWAUWASA na RUWASA kuhakikisha wa wanatatua changamoto ya maji kwa wakati ili wananchi waweze kupata maji safi na salama katika maeneo yao,wakati huohuo amewataka TANESCO kuhakikisha wanapeleka huduma ya umeme kwa wananchi na kupata umeme kwa wakati.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa,Mhe,Balandya Elikana amewataka watumishi kutumia nafasi walizo nazo kwa uaminifu mkubwa ,kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kuwapa wananchi huduma bora na stahiki ili kutimiza dhima ya Serikali ya awamu ya sita kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Veronika Kessy amesema kuwa Halmashauri imeweza kukusanya Mapato ya ndani kwa kipindi cha miaka mitatu mwaka wa fedha2019/hadi 2022 yameongezeka kutoka shilingi 2.3 sawa na asilimia mia moja na moja hadi kufikia shilingi bilioni 2.7 sawa na ongezeko la asilimia mia moja kwa mwaka fedha 2021/2022 na kipindi cha 2022/2023 wameweka Malengo ya kukusanya shilingi bilioni 3.1 sawa na ongezeko la asilimia kumi na saba ambapo kwa Mwezi Julai wameweza kukusanya kiasi cha shilingi 200,3793,000/=sawa na asilimia 7.3.
Bi Veronika Kessy ameongeza kwamba Halmashauri inandelea na uboreshaji wa ukusanyaji, usimamizi na udhibiti wa mapato kwa kutumia mashine za kiletroniki yaani Pos,Sambamba na hilo ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi imeendelea kutoa mikopo ya mapato ya ndani ya asilimia kumi isiyokuwa na riba kwa kina mama,vijana na walemavu na imeendelea kusajili vikundi kwenye mfumo ambapo kwa sasa vikundi 300 kwa mwaka 2021/2022 vimeweza kusajiliwa na zaidi Kiasi cha shilingi 200,000,000/ zimetolewa kwa vikundi 16 vya wanawake,vikundi 6 vya vijana na watu 5 wenye ulemavu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe,Alexender Mnyeti amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Adamu Malima kwa ujio wake katika Halmashauri ya Wilaya Misungwi kujitambulisha kwa wananchi na kupokea taarifa maendeleo ya miradi na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikano mkubwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Adam Malima(katikati) akiwasili katika Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Misungwi kwa lengo la kupokea taarifa ya Miradi ya maendeleo na kujitambulisha kwa Viongozi pamoja na wananchi ,Kushoto Mkuu wa Wilaya Mhe, Veronika Kessy na Nyuma ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyevaa koti jeusi ni Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Balandya Elikana na wengine ni Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo Agost 6,2022'
Baadhi wa Viongozi wa dini,Wakuu wa Idara na Vitengo na watumishi wengine wakisikiliza kwa makini na kupokea Maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Adam Malima katika ziara ya kupokea taarifa za maendeleo ya Miradi na kujitambulisha katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Agosti 6,2022.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.