Mkuu wa kitengo cha sheria ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa Bw. Muhidin Mapejo atoa wito kwa viongozi wa vyama mbalimbali kuzingatia sheria na kanuni zinazotolewa na ofisi ya ya msajili wa vyama vya siasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 24 Oktoba 2024 katika Halmashauri Wilaya ya Misungwi kilichokuwa na lengo la kuwapa elimu viomgozi wa vyama mbalimbali vya siasa na uelewa juu ya sheria kanuni na miongozo ya Ofisi ya Msajili wa vyama Taifa ambapo Bw. Muhidin Mapejo ameeleza kuwa elimu inayotolewa ni muhimu kwa viongozi hao, ili waelewe vizuri wajibu wao katika kutekeleza shughuli za chama husika na jinsi ya kujiandaa kwa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kufuata sheria ikiwa ni njia mojawapo ya kujenga amani na imani miongoni mwa wananchi kuhusu uchaguzi huru.
Kwa upande wake afisa uchaguzi Bw. Dickson Kawovela kwa niaba ya Msimamizi wa uchaguzi Bw. Addo Missama amewapongeza viongozi hao wa vyaama kwa kushiriki kikao hicho na kuamini kuwa watakua sehemu ya kutoa elimu walioipata kwa wagombea waliodhaminiwa na vyama hivyo katika kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa kijiji au kitongoji pamoja na wajumbe wa kamati ya kijiji au kitongoji (kundi mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) ili wawezi kufanya kampeni huru na haki zisizo na vurugu za aina yoyote ya uchochezi miongoni mwao.
Katika kikao hicho Viongozi wa vyama kutoka CCM,CHADEMA,CUF,ACT WAZALENDO walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi juu ya kanuni mbalimbali, ikiwa ni pamoja na usajili wa wagombea na taratibu za kampeni, ambapo ni fursa nzuri kwa viongozi hao kuimarisha uelewa wao na kuongeza ufanisi katika maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika Novemba 27 Mwaka huu.
Mkuu wa kitengo cha sheria ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa Bw. Muhidin Mapejo (katikati) Msaidizi wa Usajili vyama vya siasa Zanzibari Bi. Latifa Ahmed (kushoto) afisa uchaguzi Bw. Dickson Kawovela (kulia) wakiwa katika kikao na viongozi wa vyama mbalimbali kilichofanyika jana katika Halmashauri Wilaya ya Misungwi.
Viongozi wa siasa katika kikao na Mkuu wa kitengo cha sheria ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.