Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza limeridhia ombi la Serikali kupitia Wizara ya Ardhi la Kutenga na Kutoa Eneo la Ardhi takribani Hekari 1000 kwa ajili ya kuweka na kujenga Bandari Kavu katika Maeneo yaliyo karibu na Reli ya Wilaya ya Misungwi ili kuimarisha miundombinu ya Mawasiliano na Usafirishaji wa Shehena na Mizigo kuelekea katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hii,Mhe, Antony Bahebe Masele alitangaza uamuzi huo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika katikati ya Wiki hii katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Misungwi, na kueleza kwamba Madiwani wameridhia kutenga Eneo hilo na kulitoa kwa Serikali kutoka kwa Wananchi kwa ajili ya matumizi yalikusudiwa baada ya hatua na taratibu zote kukamilika kwa kuzingatia Sheria za masuala ya Ardhi ili kuweza kukuza uchumi na kuleta Maendeleo kwa Wananchi wa Misungwi na Taifa kwa ujumla.
Mhe, Bahebe alieleza na kufafanua kuhusu umuhimu wa kutoa Eneo hilo wakati hoja ya taarifa ilipowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hii kwamba mahitaji ya eneo hilo ni ya haraka kwa ajili ya Serkali kufanya maandalizi pamoja na kutenga fedha za shughuli husika ya kutengeneza Bandari kavu itakayokuwa karibu na Reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza inayopita katika baadhi ya maeneo ya Wilaya hii nakuwaomba kupisha maamuzi sahihi kwa niaba ya Wananchi.
Awali akiwasilisha hoja hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Eliurd Mwaiteleke alisema kuwa Serkali kupitia Maelekezo na Ombi la Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe Angelina Mabula aliyewasilisha taarifa ya ombi la Serikali la Kutenga Eneo lililo karibu na Reli kwa ajili ya matumizi ya shughuli za Bandari Kavu na kuomba Baraza likubali kutoa Eneo la kutosha kwa kazi hiyoambapo maeneo yanayofaa ni katika Kata ya Fella, Ukiriguru na Kanyelele.
Baraza hilo liliridhia kutenga eneo hilo mara baada ya baadhi ya Madiwani kutoa mapendekezo ya maeneo yaliyopo katika Kata zao ambapo Diwani wa Kata ya Fella, Mhe,Paulo Kishinda alipendekeza na kuridhia kugawa baadhi ya maeneo yaliyopo katika Kijiji cha Fella na kuomba taratibu zinazotakiwa zifanyike kwa kushirikisha Wananchi wa maeneo hayo,
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.