Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,Eliurd Mwaiteleke, amewataka na kuwaasa Wanafunzi wa Kike kuthamini na kufaulu vizuri katika Masomo ya Sayansi ili kujiandaa kuzitumia fursa za uwepo wa Viwanda katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kutumia taaluma ya Sayansi watakayoipata kwa maanufaa yao na hatimaye kukuza Uchumi wa taifa.
Wito huo kwa Wanafunzi hususan wa Kike ulitolewa wakati Hafla maalum ya Chakula cha Jioni kilichondaliwa na Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Misungwi ambapo Mkurugenzi Mtendaji akiambatana na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri walikula pamoja na Wanafunzi wa KIdato cha tano na Sita wakiwa na wanajumuiya, Wafanyakazi na Walimu wote wa Shule hiyo kwa lengo la kuwatakia heri na baraka katika Mitihani yao ya Kidato cha Sita mwezi Mei 2017,ambapo jumla ya Wanafunzi wa kike 44 wanamaliza masomo katika mchepuo wa CBG (26) na EGM (18),
Mwaiteleke amewasihi na kuwaombea wanafunzi hao wa kidato cha Sita kufaulu kwa kiwango kikubwa cha daraja la kwanza ili kuweza kupata fursa ya kuendelea na Chuo Kikuu na hatimaye kuhitimu masomo ya Elimu ya juu na kulitumikia taifa hususan katika nyanja na sekta ya Viwanda ambao ndio mwelekeo na dira ya nchi yetu kufikia katika uchumi wa Viwanda na Vijana wa kike ndio nguzo safi na taifa linathamini na linahitatji mchango wao na kuwaeleza kwamba Serikali inaandaa mazingira mazuri ya ajira na fursa nyingi zitatolewa kawa Wasomi hususani Vijana wa Kike.
'Wanafalsafa wanasema ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima na Taifa kwa ujumla".Alisema kwa msisitizo Mkurugenzi Mwaiteleke,na kuwaomba wanafunzi hao kumtegemea na kumtanguliza Mungu katika kila jambo na kutenga muda na ratiba vizuri ya kusoma kwa lengo la kujpata mafanikio yao jamii na taifa kwa ujumla wake.
Mkurugenzi Mtendaji,Mwaiteleke pia ,aliwaagiza Wakuu wa Shule zote Wilayani hapa kuanzisha na kuendeleza mpango mkakati wa kufanya Midahalo mbalimbali ya kujadili masuala na mambo ya kielimu ambapo utaratibu huu utawawezesha wanafunzi kupaena na kubadilishana uzoefu na kuongeza busara,maarifa na kuwa na fikra na uwezo mpana wa kupambanua mambo ya kiuchumi na kijamii na kuandaa taifa la Vijana wenye kufanya kazi kwa kutumia taaluma na Weledi mkubwa na kuelekeza Idara ya Elimu Sekondari kufuatilia na kusimamia Vizuri utekelezaji wa Midahalo
Akielezea mafanikio na maendeleo ya Shule na kitaaluma Mkuu wa Shule hiyo,Mathias Homboyo amesema kwamba maendeleo ya kielimu shuleni hapo nai mazuri akitoa mfano wa ufaulu wa Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita walifanya vizuri sana kwa mwaka 2016 ambapo matokeo ya Kidato cha Sita waliofanya mtihani walikuwa 126 na wote walifaulu katika madaraja ya Wanafunzi 120 walipata daraja la tatu hadi la kwanza na Wanafunzi 6 tu ndio walipata daraja la Nne,na kulingana na maandalizi ya Wanafunzi na walivyofundishwa na Walimu wao alisema wanamatarajio ya kufanya vizuri tena kwa mwaka 2017 na kuwasihi Vijana 82 wengine wa kike .wanaosoma kidato acha tano wafuate mfano wa wanafunzi waliowatangulia na kusoma kwa bidii na maarifa na wao kufaulu kwa kiwango kizuri.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.