Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,(Pichani akizungumza na Viongozi katika kikao cha WDC Kata ya Misungwi) Eliurd Mwaiteleke amewataka na kuwaagiza Viongozi wa Kata na Vijijiji kuhakikisha wanashirikiana na Walimu Wakuu na kuweza kulima angalau Hekari 3 hadi 5 katika maeneo ya Mashamba ya Shule kwa kutumia vyema Vipindi vya EK kwa Wanafunzi wa darasa la Nne hadi darasa la Saba kwa lengo la kujiongezea kipato Shule na kuwalea Wanafunzi katika Mazingira ya kazi na maadili na Nidhamu njema ya utendaji kazi.
Mkurugenzi Mtendaji Mwaiteleke aliwataka Walimu Wakuu kushirikiana na Watendaji wa Vijiji kuwezesha Kilimo cha Pamba na Alizeti kinafanikiwa kwa kila Shule kutumia mashamba yaliyopo na Vijiji kuhakikisha wanatoa mashamba mengine ili kupata maeneo ya kutosha kwa Kilimo
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.