Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ,Eliurd Mwaiteleke aiagiza Kamati ya Ujenzi na Manunuzi ya Kituo cha Afya cha Koromije kusimamia kazi ya ukamilishaji wa ujenzi wa Majengo matano mapema na kwa ubora na wenye kukidhi vigezo na thamani ya fedha iliyotumika.
Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya ujenzi na Manunuzi wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi huo mapema wiki hii Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi,Eliurd Mwaiteleke aliwapongeza wanakamati wote kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kusimamia mafundi na kuhakikisha ujenzi unaenda vizuri na kwa kiwango na ubora wa hali ya juu kwa kutumia mafundi wenyeji ambao wamejenga vizuri kwa kuzingatia maelekezo ya Wataalam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi,Eliurd Mwaiteleke,(Katikati)akizungumza na Wanakamati ya Ujenzi na Manunuzi ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Koromije alipotembelea na kukagua maendeleo ya kazi ya ujenzi huo.
Mwaiteleke ameridhishwa na hatua ya ujenzi unavyoendelea ambapo hadi sasa wameweza kuezeka mjaengo matatu na wanatarajia ndani ya siku 3 kukamilisha kuezeka Majengo mengine mawili yaliyobaki na kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Koromije alieleza kwamba hadi hatua ya kuezeka majengo hayo wameweza kutumia fedha shilingi Millioni 260, tu kati ya fedha ilitolewa shilling Millioni 500,na matarajio yao ni kubakisha fedha ambayo itawezesha kujenga majengo mengine watakayokubaliana.
Mafundi wa kuezeka wakiendelea na kazi ya kupaua Jengo la Wodi ya Wazazi lililojengwa katika Kituo cha Afya cha Koromije.
Mkurugenzi Mwaiteleke,amewataka Wanakamati kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti ya ukamilisha wa haraka na kukamilisha ujenzi kwa kiwango na ubora mzuri kwa kuzingatia maelekezo na miongozo mbalimbali ya Serikali ya Ujenzi wa Vituo vya Afya na kuhakisha fedha ya kutosha inabaki ili iwezesha kujenga Majengo mengine na kunusuru adha ya upatikanaji wa huduma za Afya kwa Wananchi wa maeneo husika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi (Mwenye Suti ) akiambatana na Kamati ya Ujenzi na Manunuzi kukagua Majengo matano yanayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya cha Koromije.
Serikali kupitia Wizara ya TAMISEMI imetoa fedha shillingi Millioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Majengo matano katika Kituo cha Afya cha Koromije kwa kutumia mafundi wenyeji (Local Fundis) na Halmashauri ya Wilaya imeweza kutekeleza maelekezo ya matumizi ya fedha za ujenzi huo ambapo tayari inaendelea na ujenzi wa Majengo matano ya Maabara, Jengo la Upasuaji, Jengo la kuhifadhia Maiti, Nyumba ya Mganga,pamoja na Jengo la Wodi ya Wazazi na matarajio ya kukamilisha ujenzi huo ni mwezi Septemba 2018.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.