Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,amewataka Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kutekeleza kwa Vitendo Ilani ya Uchaguzi inayoelekeza mambo yaliyoanishwa ya utekelezaji wa miradi na masuala ya maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla kwa kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,Eliurd Mwaiteleke amewataka Watendaji hao kutekeleza kikamilifu na kwa Vitendo Miradi na shughuli kwa kuzingatia kiwango na ubora na kuhakikisha thamani ya fedha inafikiwa kwenye miradi ya maendeleo na kuleta matokeo chanya na manufaa kwa Wananchi.
Mwaiteleke,alibainisha na kueleza hayo wakati wa Ziara ya kikazi aliyoifanya katika Kata tatu mfululizo ambazo ni Kata ya Kijima,Nhundulu,na Isesa kwa ajili ya kukagua na kuona hali halisi ya utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa,kwenye Kata 27 na Vijiji vyote 113 vya Wilaya hii ambapo ameshatembelea Kata 21 hadi sasa.
Mkurugenzi Mwaiteleke,katika ziara hiyo amewataka Watendaji wa vijiji,Walimu Wakuu,Waganga Wafawidhi wa Zahanati na Wakuu.wa Shule kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza vizuri Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 ambayo imeelekeza katika kuboresha na kuimarisha maen eo ya Sekta za Elimu,Afya,Maji,Ardhi na Maliasili,Kilimo na Ushirika na Umwagiliaji,Miundombinu na Ujenzi,Maendeleo ya jamii,Biashara na Uwekezaji wa Viwanda ,Misitu,Tehama na Ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na Ushuru na Kodi mbalimbali za Halmashauri na Serikali kuu.
Aliwataka Watendaji ambao hawakai katika Vituo vya Kazi kuhamia mara moja katika maeneo yao ya kazi Vinginevyo hatua kali za Kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao kwa kukiuka kanuni na taratibu za kazi,hivyo kuwa katika Vituo vya kazi ili kuweza kuwahudumia Wananchi kwa ubora na ufanisi zaidi pamoja na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha inatekelezwa kwa kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa na kukamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachokidhi vigezo vya Serikali,vile vile waweze kuzingatia sheria,Kanuni na taratibu na maadili ya kazi na utumishi wa umma na kuweza kutimiza wajibu.
Mkurugenzi Mwaiteleke, ameweza kukagua na kuona utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa majengo ya Wodi katika Zahanati ya Mwawile,mbayo imekamilika boma pamoja hali halisi ya ukarabati ana uboreshaji wa miundombinu ya Zahanati kwa fedha za RBF ambazo zinatolewa kwa masharti ya ufanisi kwa kazi ambapo Kila Zahanati ilipewa Tsh,10,000,000/= na baadhi wamezitumia vizuri na wengine hawakufanya kwa kiwango kinachotakiwa katika uboreshaji na ukarabati wa miundombinu ya Zahanati husika,aliagiza Idara ya Afya kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha hizo na kutoa taarifa iliyokamilika.
Alitembelea pia katika Shule za Msingi na Sekondari na kukagua utekeleza wa miradi mabalimbali ikiwemo ujenzi wa Vyumba vya madarasa na Vyoo pamoja na Nyumba za Walimu ambapo inaonyosha hali ya upungufu wa Vyoo kwenye Shule nyingi ni tatizo na kuwaagiza Viongozi wa Vijiji kuweka mikakati ya kuanzisha ujenzi huo,na kuweza kujenga madarasa ili kukabiliana na wingi wa idadi ya wanafunzi watakaoanza shule mwaka 2018,pia kuwezesha ujenzi wa Nyumba za Walimu kwa ajili ya kukaa Walimu watakaopelekwa kufundisha katika shule husika.
Amewataka Viongozi wote wa Vijiji na Vitongoji kushirikiana na Watendaji wa Vijiji katika shughuli zote za kuibua miradi ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kuchangia miradi hiyo kwa wakati na kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa nguvu zao kwa lengo la kuharakisha kasi ya maendeleo wilayani na taifa kwa ujumla .
Katika ziara hiyo ameweza kuambatana na maafisa wa Halmashauri kutoka Idra na Vitengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Idara ya Mipango na Takwimu,Afya,Maji,Elimu Msingi na Sekondari,Maendeleo ya jamii ,Ujenzi,Biashara na Fedha na Habari na Mawasiliano ambao wamewaza kuhamasisha na kutoa uzoefu kwa Viongozi na Watendaji wa Vijiji na Kata ili kujenga uelewa wa mambo na miradi mbalimbali inayotekelezwa vijijini.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.