Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi awahimiza Watendaji kuwa wabunifu katika Utendaji na kutekeleza Miradi ya maendeleo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkurengenzi Mtendaji Bw.Joseph Mafuru amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya maendeleo kwa siku mbili tarehe 17 na 18 Febuari 2024 katika Kata ya Fella,Kanyelele,Koromije na Mamaye ambapo amewataka Viongozi,Watendaji na Watumishi wa umma kuwa na nidhamu ya kazi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuongeza ubunifu kazini ili kuleta matokeo chanya katika utekelezaji wa shughuli na Miradi ya maendeleo.
Bw.Mafuru amefafanua na kueleza kwamba kuna idadi kubwa ya Wanafunzi ambao wanafanya kazi za kuchunga mifugo,kazi za ndani, kazi za migodini pamoja na wimbi la kupata mimba kwa Watoto wa kike hivyo, kupelekea kushindwa kumaliza masomo yao, na kuwata Watendaji wa kata,Vijiji na Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa pamoja kushirikiana na Viongozi wa Vijiji na Vitongoji kudhibiti na kukomesha tabia hiyo mbaya ambayo imejengeka katika jamii zinazowazunguka.
“Hakuna cha kisingizio kwamba mimi ni mgeni wote tutawajibika kwa matokeo mabovu kwa shule za msingi na Sekondari kwa hiyo mjiandae” alisisitiza Mkurugenzi Mtendaji Bw.Mafuru.
Amesisitiza kwamba ufaulu wa matokeo wa darasa la saba na kidato cha nne hauridhishi na hivyo kuwataka Watendaji na Walimu wote kwa pamoja kabadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa bidi ili kuleta madiliko yenye tija katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji ametoa wito kwa watumishi wa umma kushirikana kwa kufanya kazi kwa bidii na kupendana ambapo Serikali ya awamu ya sita ipo tayari kuwasikiliza changamoto na kuhudumia watumishi wake katika masula mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo upandaji wa madaraja na uhamisho na madai mengine.
Katika ziara hiyo Watendaji na Walimu wamepongeza na kushukuru kwa ujio wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwani imewapa hamasa na ari mpya ya utendaji kazi na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuleta mabadiliko makubwa na yenye tija katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Kata,Vijiji na Watumishi mbalimbali waliofika katika kikao ambacho kilifanyika Kata ya Kanyelele siku ya Jumamosi.
Baadhi ya Watumishi wakisiliza na kupokea maelekezo ya kiutendaji katika ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya kujitambulisha na kukagua Miradi ya Maendeleo katika Kata ya Kanyelele,ambapo watumishi walipata nafasi ya kuuliza maswali na changamoto zinazowakabili.
Mwonekano wa jengo la Zahati katika Kijiji cha Ibongoya A ,hali ukumilishaji mpaka sasa uko asilimia 91 na imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 21.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.