Serikali yaanza zoezi la upimaji wa ardhi na utoaji wa Leseni za makazi kwa Wananchi wa Kata ya Misungwi katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ,Afisa Ardhi na Maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Fredrick Nyoka ameeleza kwamba Serikali imeamua kuanza upimaji na kutoa Lesini za Makazi katika maeneo ambayo hayajapimwa kwenye Vitongoji ambavyo vipo maeneo ya Miji kwa maana ya kutambua na kupanga makazi vizuri na kuweza kurasimisha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi pamoja na maendeleo kwa ujumla.
Bw, Nyoka amesema kwamba katika Kata ya Misungwi Leseni hizo za makazi zitatolewa kwa Wananchi wa Vitongoji vya Masawe, Misungwi D, Misri, na Mitindo na kwamba Vitongoji hivi havikuwekwa kwenye mpango wa urasimishaji wala katika mpango wa upimaji wa Halmashauri ambapo zoezi litaendelea katika Kata zingine.
Kwa upande wake Afisa Ardhi na Upimaji kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Bi, Beatrice Gowele amewaeleza Wananchi katika Mikutano yao ya Vitongoji kwamba Leseni za makazi ni nyaraka halali ya umiliki wa ardhi chini ya kifungu namba 23 ya mwaka 1999 ambayo inatolewa na kudumu kwa muda wa miaka mitano na baadaye inahuishwa, na kueleza kwamba maeneo ya Wananchi yatakuwa na thamani zaidi mara baada ya kutolewa kwa Leseni za makazi na kupata fursa ya kukopa katika taasisi za kifedha na kuongeza mitaji kwa Wafanyabiashara.
Bi, Beatrice Gowele amesema kwamba Wananchi watapaswa kulipia shilingi elfu kumi katika akaunti ya Serikali amabyo ni gharama kwa kila kiwanja maara baada ya zoezi kukamilka na watapewa Leseni hizo za makazi na kuendelea na matumizi yao kwa kujenga Nyumba za makazi bora na Serikali itaweza kukusanya kodi ya ardhi vizuri kutokana na kuwatambua.
Naye Afisa Mipango Miji kutoka Ofisi ya Kamishina wa Ardhi Kanda ya Mwanza Bw, Athuman Simba amewataka Wananchi kujiandaa kikamilifu na kuwa tayari na zoezi hili kwa kutatua na kuondoa migogoro yote inayohusu maeneo na ardhi na kuwatahadharisha kwamba katika zoezi hilo Wataalam wa ardhi hawatahusika na utatuzi wa mgogoro bali watafanya upimaji katika maeneo ambayo hayana changamoto katikamatumizi na mipaka.
Ameongeza kuwa Wananchi ni muhimu kubainisha vizuri mipaka ya maeneo, kuweka na kutenga maeneo ya barabara, maeneo ya michezo, maeneo ya wazi, taasisi za umma, maeneo ya makanisa, ambayo katika utoaji wa Leseni za makazi yataombewa kupitia bodi za Wadhamini kwa lengo la kuepusha migogoro ya baadae.
Baadhi ya Wakazi wa Kitongoji cha Misri Kata ya Misungwi wakisikiliza maaelezo kutoka kwa Afisa Mipango Miji wa Kanda ya Mwanza Mohamed Simba (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa kutoa taarifa kwa Wananchi kuhusu utoaji wa Leseni za Makazi kwa Wananchi ambao hawajapimiwa Viwanja.
Afisa Mipango Miji wa Kanda ya Mwanza Athuman Simba akizungumza na Wakazi wa Kittongoji cha Misri wakati wa Mkutano wa utoaji wa Elimu kwa Wannachi kuhusu zoezi la utoaji wa Leseni za Makazi kwa Wananchi wa Kata ya Misungwi.
Baadhi ya Wanakamati ya zoezi la Utoaji wa Leseni za Makazi iliyochaguliwa katika Kitongoji cha Masawe B, Kata ya Misungwi ambayo inafanya kazi na WAataalam wa Ardhi wa Mkoa na Wilaya.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.