Miradi madhubuti inayotekelezwa na Serikali kupitia mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kunufaisha walengwa pamoja na jamii nzima Wilayani misungwi Mkoani Mwanza.
Hayo yamebainishwa Novemba,14,2023 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TASAF Bw.Shedrack Mziray wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali akiwa amekimbatana na Wataalamu mbalimbali kutoka ngazi ya Taifa na Mkoa wa Mwanza ambapo ameridhishwa na kupongeza miradi inayoendelea kutekelezwa na Serikali kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga miradi bora na yenye tija kwa kuwaletea Wananchi maendeleo.
Mziray amesema kuwa mradi wa Shule mpya ya Sekondari ya wasichana Mwanangwa upo katika hatua nzuri na unaridhisha na unaendana na thamani ya fedha ambayo inatolewa na Serikali, na kuwataka watendaji na wasimamizi kuhakikisha wanasimamia vizuri ujenzi wa Mradi huo kwani utakapokamilika utaleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Wilaya ya misungwi na Taifa kwa ujumla.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF inchini amesema kuwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali Kupitia TASAF katika kijiji cha Mwawile ,Mradi wa Lambo na Josho ni miradi muhimu ambayo inatoa ajira ya muda kwa walengwa wanufaika wa TASAF ambapo mpaka sasa fedha ambayo imetolewa ni Shilingi Milioni 66,835,417 na kutoa wito kwa watendaji na wataalamu kutumia vizuri fedha hizo vizuri ili kukamisha mradi kwa wakati.
Katika hutua nyingine Timu ya Menejimenti ya TASAF pia imefanya ziara ya kutembelea,kukagua na kuridhishwa na maendeleo mazuri ya Vikundi 5 vya Ujasiriamali vinavyotengeza sabuni za maji ,mche na madawa vya vyooni katika kijiji cha Mapilinga Kata ya Igokelo ambapo jumla ya fedha shilingi Milioni 21,112,925,zimewanufaisha wanakikundi hao kwa kukuza vipato vyao kwa kila mtu mmoja mmoja na kaya.
Baadhi ya Miradi ya maendeleo mingine ambayo inatekelezwa na Serikali kupita TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni pamoja na Ujenzi wa Madarasa 2, Ofisi na Matundu 6 ya vyoo katika Shule ya msingi Ntende,Nduha Ujenzi wa madarasa 2, Ofisi na matundu 6 ya vyoo,Mwanangwa Ujenzi wa nyumba ya Mwalimu 2 in 1,na Mwagimagi,ujenzi wa madarasa 2, Ofisi na matundu 6 ya vyoo.
Naye mkazi wa kijiji cha Mapilinga Kata ya Igokelo Bi, Muyanja Magesa akiongea kwa niaba ya wanakikundi wenzake ameishukuru Serikali ya awamu sita kwa kuwawezesha na kuwapatia mradi kupitia vikundi ambapo wamepata ujuzi wa kutengeneza sabuni ,hivyo itasidia kupata kipato cha kuweza kukidhi mahitaji katika familia zao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TASAF Bw. Shedrack Mziray akikagua nyaraka mbalimbali za mradi wa Josho ulipo Kijiji cha Mwawile Kata ya Nhundulu hivi karibuni
Baadhi ya Miradi inayotekelezwa na Serikali kupitia TASAF katika Kijiji cha Mwawile
Baadhi ya mwonekano wa madarasa ya Shule mpya ya Sekondari Mwanangwa iliyopo Kata ya Mabuki Wilayani Misungwi ambayo chanzo chake ni Fedha kutoka Serikali kuu kupitia Mfuko wa TASAF
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.