Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 zamrika na kuridhishwa na miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Milioni 995 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Misungwi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Mhe, Abdalla Shaib Kaim ameipongeza Wilaya ya Misungwi kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo kwa ujumla na kuwataka kuendelea kuwatumikia Wananchi kikamilifu ili waweze kupata maendeleo ya kiujamii, kiuchumi na kuinua kipato cha familia.
Mhe, Abdalla Shaib Kaim amesema kuwa Kituo cha Afya cha kitawasaidia wakazi wa Misasi kwa kuwapatia huduma Wanachi hao kwani hapo awali walikuwa wakitumia muda mrefu kufuata huduma ya Mionzi Mwanza mjini katika Hospitali ya Bugando na Sekouture hivyo itaondoa adha ya umbali.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe, Kashinje Machibya amewashukuru Watumishi na Watendaji wa Halmashauri kwa kusimamia miradi na kuhakikisha inajengwa kwa kiwango na ubora na kuwataka kuongeza ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ikiwa ni pamoja na kubuni na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani hususan katika mradi wa ujenzi wa Vibanda 10 vya Standi ya Mabasi Misungwi ambao utagharimu shilingi Milioni 75.5 hadi kukamilika na utakuwa chachu kwa Wananchi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo nla Misungwi Mhe,Alexender Mnyeti ameipongeza na kushukuru Serikiali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi ya miradi ya Maji ya Mbarika hadi Mbarika ambapo mapema wiki ijayo wataanza kuona cheche za maji yataanza kutiririka katika maeneo ya Misasi na kuweza kuwanufaisha Wananchi hao na kuwataka kuwa wavumilivu wakati Serikali inaendelea kuwaletea maendeleo hususan katika sekta ya barabara ya lami ya Mwanangwa hadi Salawe.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru ameeleza kwamba Miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Jengo la Mionzi katika Kituo cha Afya cha Misasi linalotarajiwa kugharimu fedha shilingi Milioni 68.4 hadi kukamilika ambalo kwa sasa limetumia shilingi Milioni 53 ambapo litawezesha na kuwasaidia Wananchi na kuwaondolea kero za upatikanaji wa huduma za Afya .
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Wilayani Misungwi zimekimbizwa kwa umbali wa kilomita 90.7 na zimekagua miradi 5 na kuridhishwa na utekelezaji wake na kuzindua, kufungua, pamoja na kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi vyumba 6 vya madarasa Shule ya Sekondari Idetemya, Mradi wa ufugaji wa Kuku wa Mayai wa Agroberg, Mradi wa Kikundi cha cha Vijana kazi cha usafirishaji wa Abiria Ngudama –Bulemeji, Ujenzi wa Jengo la Mionzi Kituo cha Afya Misasi, na Ujenzi wa Vibanda vya Standi ya Mabasi Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.