Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakabidhiwa mashine 85 aina ya Planta kwa ajili ya upandaji wa mbegu za mazao mbalimbali Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mhe, Abdi Makange Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi amewataka wakulima kuchangamkia fursa katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha wananufaika na kutumia mvua za msimu ilikuzalisha mazao kwa tija.
Mhe,Abdi Makange Katibu Tawala Wilaya ameyasema hayo 7,Agosti,2023 katika Ukumbi wa Halmashauri wakati wa hafla ya kukabidhi planta 85 vilivyotolewa na mradi wa Beyond Cotton kwa ufadhili wa nchi ya Brazil pamoja na Shirika la chakula duniani kwa kushirikiana na TARI Ukiriguru.
Aidha Mhe, Makange alieleza kwamba wakulima wa kata tatu zilizopo katika Wilaya hiyo zitaanza kunufaika na vifaa hivyo na kuahidi kutatua changamoto ya mbolea wilayani humo ili wakulima waweze kupata mazao bora.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Dkt, Chrispine Shami amesema wakulima wamekuwa wakipata changamoto wakati wa kupanda mbegu kwa kutumia mikono hivyo kwa sasa watapanda mbegu kwa kutumia planta ambapo zitatumika kupanda mbegu hizo kwa haraka na urahisi na kupanda eneo kubwa.
Mshauri wa mradi wa Beyond Cotton Bw, Castory Kabiki amesema vifaa hivyo vimenunuliwa kwa Tsh, 450,000/= kila moja ambazo ni sawa na Tsh, 38.250,000/= ambapo lengo la ugawaji ni kuhakikisha vinawapunguzia gharama wakulima za kulima na upandaji wa mbegu.
Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Mhe, Kashinje Machibya alitoa pongezi kwa upatikanaji wa vifaa hivyo kwani uwepo wa mradi wa Beyond Cotton umekuwa kipaumbele kutoka kwa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan ambapo kwa sasa inawafikia wakulima.
Wakati huo huo Elias Mathias mkazi wa Kijiji cha Igongwa Kata ya Sumbugu kwa naiba ya wakulima wenzake ametoa shukrani za dhati ambapo alieleza kwamba vifaa hivyo vitarahisisha upandaji kwa muda mfupi na kuahidi kutoa elimu hiyo ya namna ya upandaji kwa wakulima wengine.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw,Abdi Makange akifanya jaribio la kupanda mbegu za maharage kwa kutumia mashine ya Planta jana wakati wa ugwaji wa mashine hizo Wilayani Misungwi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw,Abdi Makange akiwa ameshikana mkono na mmoja wakulima wakati wa kukabidhi mashine za Planta katika Ofisi za Halmashauri na wa pembeni kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt Crispine Shami.
Baadhi wakulima wakisikiliza na kutoa maoni yao wakati wa ugawaji wa vifaa vya upandaji mbegu aina ya Planta ambapo zoezi hilo lilifanyika jana katika Ofisi za Halmashauri Wilaya ya Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.