Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ,Juma Sweda amewataka Wananchi na Wakulima Wilayani hapa Kulima Kilimo cha Mazao yanayostahimili Ukame na kuzitumia kikamilifu Mvua za Masika zinazoendelea kunyesha hivi sasa ikiwa ni kukabiliana na uhaba na Upungufu wa Chakula unaoonekana kuwakumba baadhi ya Wananchi, kutokana na kuchelewa kunyesha Mvua za Vuli kwa Mwezi Novemba 2016 hadi Januari 2017.
Mkuu wa Wilaya huyo alibainisha hayo na kueleza mikakati ya Wilaya katika Shughuli za Kilimo alipowatembelea Wakulima wa Kijiji cha Mondo katika Kata ya Mondo kwa Lengo la kuhamasisha Kilimo cha Mazao yanayoistahimili Ukame ya MTAMA, VIAZI na ALIZETI ambapo alishiriki Kulima na Wakulima hao kwa Kutumia Jembe la kukokotwa na Ngombe PLAU katika Shamba la Mfano Hekari zaidi ya mbili la Mkulima Mmoja wa kijiji hicho cha Mondo.
Amewataka pia Wananchi wenye Mifugo kuuza baadhi ya Mifugo ili kuweza kujikimu kimaisha pamoja na kununua Chakula cha Familia ili kongeza na kuleta tija katika Shughuli za Maendeleo
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.