Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda awaagiza Madiwani wa Halmashauri ya Misungwi kufuatilia na kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata na vijiji.
Mkuu wa Wilaya huyo ametoa agizo hilo mapema jana wakati wa Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambapo katika Mkutano huo ulimchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Madiwani hao wameapishwa rasmi kuwa Madiwani na wanapaswa kuanza majukumu yao mara moja.
Juma Sweda amewaagiza Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuanza kazi ya kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa , ujenzi wa vyoo, ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya pamoja na miradi mingine.
Amewataka kuanza kufanya vikao na Wananchi ili waweze kujadili mambo ya maendeleo na kuweka mipango mikakati ya kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo ambayo imeanzishwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali pamoja na michango na nguvu za Wananchi na kuhakikisha inatekelezwa kwa kiwango na ubora na inakamilika kwa wakati.
Amewapongeza pia Madiwani hao kwa kuaminiwa na Wananchi na kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Madiwani na kuwaomba kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 hadi 2025 kwa kasi ili kuwaletea Wananchi maendeleo ya dhati na kuongeza kipato na kukuza uchumi wa taifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri, Kashinje Machibya amewashukuru Madiwani kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi kwa kipindi cha miaka mitano na na kueleza kwamba binafsi ataongoza na kufanya maamuzi ya pamoja kwa kushirikiana na kuwaomba watoe ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu ya kusimamia shughuli za Serikali na kwamba ana matumaini makubwa na Watendaji na Watumishi wa Halmashauri.
Kashinje Machibya ameahidi kusimamia Halmashauri na kuhakikikisha Halmashauri inapata Hati safi kwa kila mwaka kwa kufuata miongozo na sheria zilizopo na kupitia kwa Watendaji watahakikisha wanaweka mipango mizuri ya maendeleo.
Amewataka Madiwani hao kufanya kazi kwa umoja na mshikamano pamoja na matarajio makubwa ya kupewa ushirikiano mkubwa kutoka kwa Watendaji na Watumishi wa Halmashauri kwa kuzingatia sharia kanuni na taratibu za Serikali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Misungwi, Kisena Mabuba amewasilisha taarifa ya shughuli za Serikali zilizotekelezwa na Halmashauri kwa kipindi cha kuanizia mwezi Mei hadi Novemba 2020, na kueleza kwamba shughuli hizo zimetekelezwa na Menejimenti ya Halmashauri ambapo utekelezaji wa miradi na shughuli umefanyika katika Idara na Vitengo vya sekta zote.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kashinje Machibya akizungumza katika Mkutano wa Braza la Madiwani mara baada ya kuchaguliwa kuongoza Halmashauri hiyo katika Ukumbi wa Halmashauri mapema jana.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Rahma Emmanuel Fidel akiomba kura kwa Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Misungwi kabla ya kuchaguliwa kwa kura zote 36 za ndiyo kuwa Makamu Mwenyekiti wa Hamashauri ya Misungwi.
Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri ya Wilaya ya Misungwi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kuanzia mwezi Mei hadi Novemba 2020 kwatika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmsahuri.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.