Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Miradi mbalimbali inayosimamiwa vizuri na Menejimenti kwa kutumia Force Akaunti iliyojengwa kwa kiwango na ubora na kuzingatia thamani ya fedha .
Akizungumza katika Ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo,Makamu Mwenyekiti wa Halm ashauri Mhe,Paulo Kishinda alieleza namna alivyoridhishwa na ujenzi na kuwapongeza Waatalam wa Halmashauri kwa kuweza kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa kupitia Kamati za Shule,Kamati za ujenzi na manunuzi kwa ushirikiano wa Wahandisi wa Ujenzi na Kitengo cha Ugavi na Manunuzi kwa kutumia Mafundi wazawa (Local Fundis) ambao wamejenga kwa ubora na kiwango kikubwa na miradi imekidhi vigezo kulingana na thamani ya fedha iliyotumika.
Makamu Mwenyekiti,Mhe,Paulo Kishinda alisema hayo mara baada ya kutembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Walimu( Six in One ) iliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Isakamawe katika Kata ya Kijima ambayo itagharimu shillingi 141,000,000 fedha ambazo ni ufadhili wa Shirika la Elimu Tanzania zilizotolewa kwa awamu mbili ya shilingi 70,500,000 kwa kila awamu,fedha hizo zimetolewa ili kuweza kuboresha na kuleta ufanisi wa utendaji kazi kwa Walimu kwa kuwa na makazi mazuri na bora.
Akitoa maelezo kwa Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango,Kaimu Mhandisi wa Ujenzi,Revocatus Bulahya alisema kwamba ujenzi huo umefanyika kwa ushirikiano wa Waatalam wa Halmashauri pamoja na Kamati ya ujenzi ya Shule ambapo walikuwa wanafanya manunuzi ya vifaa vya ujenzi moja kwa moja Madukani na kuweka stoo na kuendelea kumsimamia Fundi ujenzi na kutoa ushauri mara kwa mara kulingana na Mkataba na kwa sasa wanaendelea na hatua ya ukamilishaji wa ujenzi huo ambapo wanatarajia kumaliza ujenzi mwezi Disemba mwaka huu.
Ujenzi wa Mashimo ya Maji machafu ya Choo yanayojengwa katika Nyumba ya Walimu Six in One Sekondari ya Isakamawe.
Kaimu Mhandisi wa ujenzi,Bulahya alieleza kuwa Fundi ujenzi anaendelea kuchimba mashimo ya maji machafu matatu,kukamilisha upigaji wa lipu na kuweka dari, vigae,vioo pamoja na kupiga rangi ndani na nje ya jengo na manunuzi ya Vifaa vya ukamilishaji yameshafanyika hivyo wataendelea kusimamia kikamilifu ili kuweza kufanya ukamilishaji bora na wenye viwango, Alisisitiza Bulahya.
Kamati hiyo iliweza pia kukagua Mradi wa ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vitatu vya Madarasa ya Wanafunzi wa Kidato cha tano na Sita katika Shule ya Sekondari Misasi kwa gharama ya shilingi 30,000,000 ambapo ukamilishaji wa ujenzi umefanyika vizuri na unaendelea kukamilika kwa kuweka Vioo na Vigae na wamejenga kwa kutumia Local Fundis na kusimamiwa na Kamati ya ujenzi ya Shule kwa kushirikiana na Waatalam wa Idara ya ujenzi,Ugavi na Manunuzi na majengo yamekamilishwa vizuri.
Vioo katika Sekondari ya Misasi
Aidha,Kamati ilikagua Mradi wa ukarabati wa majengo matano ya vyumba vya madarasa yanayoendelea kukarabatiwa katika Shule ya Sekondari Misasi kwa fedha zingine 30,000,000 zilizotolewa na Serikali kuu kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia mashuleni, ili kuweza kuinua kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi wa Sekondari na kazi ya ukarabati huo inaendelea vizuri na ipo katika hatua ya ukamilishaji.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Wataalam wa Halmashauri wakisikiliza maoni na ushauri kutoka kwa Mhe,Ngwanza Nyahehe (katikati) kuhusu utekelezaji wa miradi ya ujenzi kwa kutumia mafundi Wazawa.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ,Mhe, Kishinda aliishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe,Rais Dkt, John Pombe Joseph Magufuli kwa kubuni na kuleta Mpango na Sera ya kutumia Force Akaunti katika ujenzi wa Majengo ya Serikali na kueleza kwamba imesaidia sana na kuwezesha kujenga majengo zaidi kwa gharama kidogo na kupata ziada ya fedha ambazo zitafanya kazi zingine, akitolea mfano ujenzi wa Jengo la Bima ya Afya( OPD) mradi ambao unaendelea kukamilishwa ambapo hadi sasa umegharimu fedha shilingi 141,525,250 na ujenzi umefanyika kwa kiwango kikubwa, Alifafanua Makamu Mwenyekiti,Mhe Kishinda.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.