Mabalozi wa Jinsia na Lishe na Wataalam wa Sekta ya Mifugo na maendeleo ya jamii wapatiwa mafunzo ya namna ya kuongeza ufanisi wa Usindikaji na Uzalishaji wa Maziwa Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mafunzo hayo yametolewa leo 27, Machi, 2024 na Mratibu wa Kitengo cha Jinsia Lishe Shirika la Heifer International Bi.Nyamate Msobi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halamshauri ya Wilaya ya Misungwi ambayo yalihusisha kuwajengea uwezo maafisa mifugo, Maafisa ushirika ,Maendeleo ya Jamii,Lishe na Mabalozi kwa lengo la kutambua namna bora ya ukuanyaji maziwa kupitia uboreshaji wa miundombinu ya kukusanyia maziwa na kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa.
Amesema kuwa mafunzo hayo ambayo wameyapata washiriki yatasaidia kuongeza uelewa wa juu ya dhana za kijinsia na jinsi zinazohusiana na maendeleo,na kuona umuhimu wa jinsia katika Maisha ya kila siku ya ufugaji na kutambua mwuafaka wa kijinsia katika kuboresha ushiriki wa wanawake katika maamuzi ngazi ya kaya na jamii kwa ujumla.
Bi.Nyamate ameeleza kwamba ushirikishwaji wa Wanawake katika jamii utawezesha kuongeza kufanya maamuzi katika kipato cha familia, kushiriki katika maamuzi ya kuongeza uzalishaji wa maziwa katika ngazi ya kaya pamoja kuongeza wigo wa wanawake kupata fursa za kiuchumi na kuongeza ushiriki wa wanawake na wanaume katika majukumu mbalimbali na hivyo kuchangia uwepo wa uhakika wa chakula katika kaya na jamii.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamiii Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza Bi. Janeth Shishila amesema kuwa mafunzo walioyapata yakawe chachu ya kuleta mabadiliko ya kifikra katika jamii zinazowazunguka kwa kuwaelimisha na kuwawezesha wanawake kupata fursa sawa kama wanaume katika kuzalisha uzalishaji na hivyo kupunguza njaa katika jamii.
Bi.Shishila ameongeza kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa kujumuisha masuala jinsia na lishe kwa wanawake na wanaume itasaidia uhakika wa chakula na lishe na kuongeza upatikanaji wa rasilimali miongoni mwa wanawake ,hivyo kupelekea kuboresha lishe na afya ya familia.
Naye Kaimu Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Johnbosco Nkunguu ametoa wito kwa Wataalamu wa Mifugo na Mabalozi wa jinsia na Lishe kuendelea kutoa mafunzo kwa vikundi walivyoviunda,wasikate tamaa katika kuwaelekeza vikundi vya wafugaji na kuwataka kundelea kuwajengea uwezo na kuwapa moyo pindi taratibu zitakapo kamilika na kukidhi vigezo watapewa mkopo wa ng’ombe wa maziwa.
Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa maziwa Tanzania (TI3P) umeendelea kutoa mafunzo ya Jinsia na Lishe katika ngazi ya jamii ili kuleta mabadiliko chanya katika sekta ndogo ya maziwa kupitia uhamasishaji wa uwekezaji kutoka sekta ya umma na binafsi kwa lengo kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa, ikiwa kauli mbiu ni” Maziwa maziwa dhahabu nyeupe,maziwa salama chakula na fedha”
Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa makini kikao cha mafunzo kutoka Mradi Shirikishi wa Wasindikaji,Wazalishaji wa Maziwa Tanzania kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri leo mapema ambapo wadau pamoja na wataalamu waliweza wapatiwa mafunzo ya namna ya kuongeza ufanisi wa Usindikaji na Uzalishaji wa Maziwa.
Mratibu wa Kitengo cha Jinsia Lishe Shirika la Heifer International Bi.Nyamate Msobi akitoa mafuzo leo ya namna ya kuongeza ufanisi wa usindikaji na uzalishaji wa maziwa katika ukumbi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.