Kituo cha Uchunguzi na Upimaji wa kubaini mahitaji Maalumu ya Ujifunzaji kwa watoto wenye Ulemavu chazinduliwa katika Shule ya Msingi Maalumu ya Mitindo Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza.
Hayo yamejiri wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho ambapo Mkurugenzi wa Elimu Maalumu Wizara ya Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Dkt ,Magreth Matonya ambaye alimwakilisha Kamishina wa Elimu nchini kwa ajili ya Uzinduzi wa Kituo hicho ambacho kitatumika na kubaini kiwango cha watoto wenye mahitaji maalumu ya ujifunzaji kwa watoto wenye ulemavu katika Shule ya maalumu ya Mitindo Kata ya Misungwi Wilayani humu.
Dkt, Matonya amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassani ina mikakati mikubwa yakujenga kituo kikubwa cha upimaji mkoani Dodoma ambapo mchakato wake umeenza na kitakuwa kinatumika kupima watoto wenye mahitaji Maalumu pamoja na usambazaji vifaa mbalimbali nchi nzima kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa akili,uziwi na ulemavu wa kutoona.
”Kwa Serikali kuona umuhimu wake imeanzisha vituo vya Upimaji katika ngazi za Halmashauri na leo tuko hapa Misungwi”. Alisema Dkt. Matonya.
Matonya ametoa rai kwa shule zote za serikali, binafsi na Shule za kanisa kwa Wakuu wa Shule na walimu wakuu waweze kubaini watoto wenye mahitaji maalumu na kuajiri walimu wenye sifa za kufundisha watoto hao na kuwabaini watoto wenye changamoto ili waweze kupatiwa huduma stahiki.
Vilivile, amewataka Wazazi wenye wototo wenye mahitaji maalumu wawaruhusu watoto wao kujitokeza katika zoezi la ubainishaji na wahakikishe watoto wanabainishwa na kurejeshwa shuleni ili kupata Elimu kulinga na kiwango chao.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw,Benson Mihayo amesema Halmashauri ya Misungwi iko tayari kushirikiana na Wadau mbalimbali katika Sekta ya Elimu na Mashirika binafsi kwa lengo kuinua kiwango cha Elimu katika Wilaya ya Misungwi, pamoja na hayo ametoa rai na kuwataka wadau wote kuendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kielimu pamoja na kulinda miundo mbinu iliyopo kwa ajili watoto wenye mahitaji maalumu.
Kwa upande wake Afisa Elimu Maalumu wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Charles Pamba amesema kuwa kuzinduliwa kwa Kituo cha uchunguzi na upimaji kwa watoto wenye mahitaji maalumu ni muhimu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na ni jukumu la walimu kuweza kutafuta njia sahihi za kumsadia mtoto katika kujifunza na kutumia zana zinazokubalika katika ujifunzaji na kusisitiza kwamba mwaka huu wamekadiria kusajili watoto zaidi ya 60 na kwa Wilaya nzima watoto wenye mahitaji maalumu wapo 615 ambao tayari wamekwisha kuandikishwa.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maalumu ya Mitindo Bw.Wilson Machiya amelishukuru Shirika hilo la Sense international na ADD International Foundation kwa kuweza kuanzisha Kituo cha Upimaji katika shule ya Msingi Maalumu ya Mitindo ambapo kupitia kituo hicho kitasaidi zoezi la kupima na kubainisha watoto wenye mahitaji maalumu.
Hata hivyo Bw.Machiya amesema kwepo kwa mafunzo hayo yatasaidia upimaji na ubainishaji kwa watoto wenye mahitaji maalumu hivyo kazi upimaji kuwa nyepesi kutoka na mafunzo waliyoyapata kutoka kwa viongozi wao.
Baadhi ya Viongozi( wa kwanza kushoto ni Kaimu DED Misungwi ,Bw.Benson Mihayo na aliyevaa koti jeusi ni Mkurugenzi wa Elimu Maalumu TAMISEMI Dkt Magreth Matonya),wakishuhudia zoezi la uzinduzi wa jengo maalumu kwa ajili ya uchunguzi na Upimaji wa watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Shule ya Msingi Mitindo hapo jana.
Baadhi ya Wawakilishi wa Vyama vya Walemavu na washiriki mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa kituo Maalumu cha Uchunguzi na Upimaji wa Watoto wenye Ulemavu katika Shule Maalumu ya Msingi Mitindo wakimsikiliza mgeni rasmi.
Muonekano wa Jengo maalumu litakalotumika kwa ajili ya Uchunguzi na upimaji wa Watoto wenye Mahitaji Maalumu katika Shule maalumu ya Mitindo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.