Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahili Geraruma ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwa utekelezaii mzuri wa Miradi ya maendeleo yenye thamani ya Bilioni 3.1.
Ametoa pongezi hizo mapema jana wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 zikiwa katika Halmaashauri ya wilaya ya Misungwi ambazo zilikimbizwa na wakimbiza Mwenge waliweza kukagua Miradi saba yenye thamani ya Bilioni 3.1 ambapo miradi 3 iliwekewa jiwe la msingi, na miradi 4 ilizinduliwa na yote imegawanyika katika sekta ya elimu, Afya, barabara, Maji na uwezeshaji Wanachi kiuchumi.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 akikagua mradi ujenzi wa Shule ya Sekondari Manawa amewataka Viongozi kusimamia kikamilifu na kuhakikisha Wataalam wanafanya marekebisho ya kasoro na mapungufu yote yaliyobainika ikiwa ni pamoja na kufuata na kuzingatia kanuni taratibu za ujenzi ili kukamilisha Ujenzi na kupata miradi inayokidhi ubora na yenye viwango
Wakati huo huo aliagiza kufanyika vizuri kwa skiming pamoja kuongeza vigae kwenye vyumba vya vyoo na kushauri kuweka sawa muundo wa Kamati za ujenzi, Kamati za Manunuzi na mapokezi kuongozwa na Wataalam ili kuweka takwimu sahihi na utunzaji mzuri wa Nyaraka.
Wakizungumza na vyombo vya Habari baadhi ya Wananchi wa Kata ya Misasi na wanufaika wa Shule ya Sekondari ya Manawa wameeleza na kutoa shukrani kwa Mhe, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Milioni 470 za kujenga Sekondari ambayo itapunguza kero ya elimu iliyokuwepo kwa Wanafunzi kutembea umbali mrefu na kuzorotesha taaluma na kushauri Serikali kuweka miundombinu ya bweni katika shule hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Veroika Kessy ameeleza kwamba Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 zitakimbizwa kwa umbali wa kilomita 75.2 ambapo utapitia na kukagua miradi 7 katika miradi hiyo mchango wa jamii ni shilingi Milioni 11.3 na Halmashauri imetoa shilingi million 16.7 ambapo Serikali kuu imechangia million 1.6 na Wahisani wamechangia shilingi million 1.5 na miradi yote imetekelezwa kwa kiwango na ubora.
Miradi hiyo iliyowekewa mawe ya Msingi na kizinduliwa ni pamoja na Ujenzi wa Shule ya Sekondari Manawa , ujenzi wa barabara ya lami kilomita 1, ujenzi wa Kituo cha Afya Usagara ,Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Afya MacWish, Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji Maji Fella, Ujenzi wa madarasa 8 katika shule ya Sekondari Sanjo na Mradi wa Kikundi cha Vijana cha usafi wa mazingira na usafirishaji mizigo .
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.