Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa Majaliwa amewaahidi Wananchi wa Jimbo la Misungwi kuendelea kuimarisha na kuleta neema katika Sekta ya maji, pamoja na miumdombinu ya barabara Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza.
Mhe, Kassim Majaliwa ametoa ahadi hizo kwa Wananchi wa Wilaya ya Misungwi wakati akinadi Sera na Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika Viwanja vya Amani katika mwendelezo wa Kampeni za kuomba kura za mgombea Urais, Ubunge na Udiwani kupitia CCM, na kuwataka Wananchi hao kuwa makini na kuchagua Viongozi wanaofaa na wanaoweza kuwaletea maendeleo ya dhati.
Mhe, Majaliwa alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitano imeleta fedha nyingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuanzia mwaka 2015, na fedha hizo zimetekeleza miradi ya sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya maji, Kituo cha Afya na Mradi wa Hospitali na miradi ya miundombinu ya barabara za lami mjini Misungwi, “ wakati huo huo ameahidi kushughuikia suala la upungufu wa pampu ya kusukuma maji katika mradi wa Maji wa Nyahiti –Misungwi, ambapo amemtaka Mbunge Mteule wa Jimbo la Misungwi mara baada ya kuapishwa Bungeni aanze kulitatua kwa haraka ili Wanannchi wapate maji ya kutosha”, alisisitiza Mhe, Majaliwa.
Naye Mbunge Mteule wa Jimbo la Misungwi, Alexander Mnyeti amewahakikishia Wananchi wa Jimbo hilo kumwamini na kuwaahidi kuchapa kazi kwa kasi na kuwatumikia kikamilifu kwa kuibadilisha Wilaya ya Misungwi kwa kuwaletea maendeleo zaidi kupitia sekta ya Afya, Elimu, Maji na miundombinu ya barabara pamoja na kuondoa kero mbalimbali zinazokwamisha maendeleo, na kuwaomba Wananchi wote kwa pamoja mwezi oktoba mwaka huu 2020 kumchagua Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt, John Pombe Magufuli ili aendelee kuwaletea Wananchi maendeleo makubwa kwa miaka mitano tena.
Mhe Kassim Majaliwa , Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa akisalimiana na Viongozi wa ngazi ya Wilaya akiwemo Katibu wa CCM Wilaya Latifa Malimi (kulia )
Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Misungwi, Daud Gambadu wakati akitoa salamu na kumkaribisha Mhe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa katika Jimbo la Misungwi na kumwahidi kwamba Wananchi wa Wilaya ya Misungwi wameamua na wana jambo lao tarehe 28 oktoba mwaka huu ambalo ni kumchagua kwa kura zote Dkt, John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano sambamba na Mbunge na Madiwani wote wa Kata 27 wa CCM ambao wamepita bila kupingwa.
Mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, akiteta jambo na Mbunge Mteule wa Jimbo la Misungwi, ALexander Mnyeti (kulia) wakati wa kunadi Sera na Ilani ya CCM Viwanja vya Amani Wilayani Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.