Kamati ya Ulinzi na Usalama yawataka Wazazi kuhakikisha Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanapata Chakula wakati wa shule Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni yaliyokamilika Wilaya ya Misungwi.
Bw. Makange amefafanua kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo na Wilaya ya Misungwi ilipatiwa Bilioni 1.8 amabazo zimetekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa, majengo ya utawala, majengo ya TEHAMA katika shule za Msingi za Mwabebea, Shilabela, Iteja pamoja na ujenzi wa Mabweni 2 katika Shule ya Sekondari za Mwambola na Misungwi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru ameeleza kwamba pamoja na watendaji watahakikisha wanasimamia na kuitunza miundombinu kikamilifu pamoja na Miradi yote ambayo inatekelezwa na Serikali kukamilika kwa wakati ili iwe manufaa kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Naye, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ametoa rai kwa Viongozi na Watendaji kuendelea kutoa elimu na hamasa kwa Wananchi na Wazazi kuendelea kuchangia chakula shuleni ili wanafunzi waweze kupata mlo kamili wawopo shuleni.
Bi.Kuboja amefafanua kwamba wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni 8238 na walioripoti mpaka sasa ni wanafunzi 7161 ambayo ni sawa na asilimia 86.5 na kufikia 28,Februari Mwaka huu wanafunzi wote watakuwa wameripoti shuleni,na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuhamasisha Watoto kuripoti shuleni kwa wakati.
Wakati huo huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shilabela Bw. Twaha Hussen ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya maendeleo ambapo mpaka sasa Serikali imejenga shule mpya ya Msingi Shilabela ambayo imechukua wanafunzi zaidi 1000 kutoka shule ya Msingi Mbela ambayo ndiyo shule mama na hivyo kupunguza msongamano kwa wanafunzi.
Erine Bosco ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Sekondari Misungwi ameishukuru Serikali kwa kuwajenga shule nzuri yenye mazingira mazuri ya kujifunzia na kuiomba Serikali ilete fedha kwa ajili ya kujenga uzio katika shule hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.