Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Misungwi imefurahishwa na kuridhishwa na Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea kujengwa katika Halmashauri ya Misungwi kwa kutekelezwa kwa kuzingatia na kufuata kiwango na ubora .
Akizungumza katika Ziara ya Kamati hiyo iliyofanyika hivi karibuni,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya,Daudi Gambadu alisema, Kamati kwa ujumla imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo inatekelezwa na Serikali ya awamu nya tano na kuipongeza Menejimenti ya Halmashauri kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa shughuli za miradi ambayo imeanishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 - 2020.
Alieleza kwamba Kamati imeona namna Ilani ya CCM inavyotekelezwa na Serikali na wameridhika kwamba shughuli zinatekelezwa vizuri ikiwemo miradi ya maij,Sekta ya Afya ,na Sekta ya Elimu ambayo inaendelea kujengwa kikamilifu na Watendaji kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya kwa usimamizi na ufuatiliaji wake mzuri uliowezesha miradi kuwa imara na yenye ubora.
Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Ngeleka lililojengwa kwa Ufadhili wa Mdau wa Maendeleo James Ngelela.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Wilaya ya Misungwi, Daudi Gambadu alieleza kwamba kwa ujumla miradi yote iliyotembelewa na Kamati hiyo imetekelezwa kwa kiwango na ubora na imezingatia taratibu za ujenzi na kuipongeza Menejimenti kwa kusimamia miradi vizuri na kuwataka kuendelea kutekeleza kikamilifu na kukamilisha miradi ambayo haijakamilika kwa wakati na ubora zaidi ikiwa ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Jengo la Upasuaji linalojengwa katika Kituo cha Afya cha Mbarika
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda aliwataka Watendaji wa Halmashauri kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa kila Sekta ili kuweza kuwapatia Wananchi maendeleo ya dhati na kunufaika na raslimali za nchi kwa taifa la Tanzania,
Alisema Miradi inayotekelezwa ni pamoja na MIradi ya Maji ambao ni wa Ngaya -Mbarika unaoendelea kutekelezwa na utaweza kutoa huduma ya maji kwa Wakazi wengi wa Kata ya Mbarika hadi Sumbugu na pia Mradi wa Afya wa ujenzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya cha Mbarika.
Mkuu wa Wilaya Juma Sweda amewataka Wananchi kuitunza na kuilinda Miradi hiyo mara itakapokamilika ili iweze kudumu na kuwanufaisha na kuweza kupata maendeleo ya Kiuchumi na kijamiii na kuondoa umasikini kwa Watanzania.
Akielezea kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahuri ya Misungwi,Eliurd Mwaiteleke alisema kwamba Menejimenti imeweza kusimamia miradi hiyo na kueleza kuwa jukumu la Watendaji wote Serikalini ni kufanya kazi kwa weledi na kuwajibika kwa kila nyanja ili kuweza kuwaletea Wananchi maendeleo kupitia miradi mbalimbali ikwemo Sekta ya Afya ,Elimu na Sekta zingine za miundombinu ya barabara na maji.
Mradi wa ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi linalojengwa katika Kituo cha Afya cha Misasi.kwa nguvu za Wananchi,Wadau na Ufadhili wa Serikali ya Irelend .
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.