Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Misungwi yaridhishwa na kupongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kupitia fedha za Serikali kuu, Wafadhali na mapato ya ndani kwa mwaka 2024/2025 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika ziara ya siku mbili ya Kamati ya Siasa ya kutembelea, kukagua na kuona miradi ya maendeleo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Misungwi Bw. Mwita Nyaingi Nyarukururu amesema kwamba miradi mingi ni mizuri na imetekelezwa kwa kiwango na ubora na kuwapongezi Viongozi wa ngazi ya Wilaya na Watendaji wote wa Serikali kwa utekelezaji na usimamizi mzuri ambapo miradi inaendelea vizuri na mabadiliko ni makubwa sana katika miradi ya sekta zote za Afya, Elimu, Maji, barabara, na Sekta ya maendeleo ya jamii na kuwataka Viongozi wa Serikali kuhakikisha wanatatua na kuondoa changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza katika baadhi ya miradi michache ili kuongeza ustawi na kuwaletea Wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya kwa ujumla wamepongeza shughuli za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilayani Misungwi wameeleza kwamba Wananchi wa Wilaya ya Misungwi wanashauku na kiu kubwa ya kuona huduma za kijamii zinaboreshwa na wananufaika na miradi inayojengwa kupitia usimamizi wa Viongozi na Watendaji wa Serikali na kuwasihi kuendelea kutekeleza miradi kwa weledi ,uadilifu na kuhakikisha inakamilika kwa ubora na kwa wakati.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Misungwi amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi ambapo Watendaji wameendelea kutekeleza kwa kuzingatia taratibu, sharia na kanuni na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango na kuwataka Wananchi wote kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya sita.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Misungwi Bw. Leonidas Kondela ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwapongeza Viongozi wote Serikali pamoja na Watendaji kwa juhudi wanazofanya katika kutekeleza miradi kupitia fedha za awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwaomba Wananchi waendelee kuumunga mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kwaletea maendeleo ya dhati Watanzania.
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Misungwi katika ziara hiyo imeambatana na Wakuu wa taasisi za Umma, Wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri na imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za msingi na Sekondari , ujenzi wa Nyumba za Watumishi, ujenzi wa miundombinu katika Zahanati na Vituo vya Afya, ujenzi wa Madaraja na matengenezo ya barabara, ujenzi wa miradi ya Maji ya bomba na Visima, ujenzi wa Mabweni ya Wasichana unaoendelea katika Shule ya Sekondari Misungwi na Mbarika, pamoja na ujenzi wa Jengo la Mahabusu ya Watoto Bukumbi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.