Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Mwanza yaridhishwa na kupongeza utekelezaji wa Miradi ya sekta ya Elimu na Miundombinu ya ujenzi wa Barabara inayoendelea kutekelezwa Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Rais,Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuboresha na kukuza Uchumi wa Wananchi imeendelea kuleta neema katika sekta ya Elimu, Maji na miundombinu ya barabara kwa kutoa fedha za kujenga miradi na hatua za ukamilishaji zinaendelea vizuri.
Wakikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara yenye mita zaidi ya mita 800 iliyojengwa kwa kiwango cha Changarawe katika Kata ya Usagara kwa gharama ya zaidi ya Milioni 110 Wilayani Misungwi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe, Michael Masanja (SMART) amesema kwamba Wananchi wa maeno ya Usagara na Wilaya ya Misungwi wanaendelea kunufaika na miradi ya Serikali ya awamu ya sita.
Wakati huo huo, Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza pia wamekagua ujenzi wa Mabweni katika Shule ya Sekondari Misungwi nakuonyeshwa kufurahishwa na ujenzi wa mabweni hayo ambapo aliwaagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi kuhakikisha wanaweka miundombinu ya Nishati ya umeme katika bweni hilo lililojengwa katika Shule ya Sekondari ya Misungwi na ametoa ahadi ya kuwapatia Seti moja ya Luninga (Television) ili kuwawezesha Wanafunzi hao kujifunza na kupata taarifa mbalimbali za maendeleo ya nchi na kimataifa.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Johari Samizi ameishukuru Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza kwa kufanya ziara na kukagua maendeleo ya miradi katika Sekata ya maji, Miundombinu ya barabara na Sekta ya Elimu msingi na Sekondari na kuwaomba waendelee kufanya ufuatiliaji huo ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati.
Baadhi ya Miradi ikiwemo Mradi wa Maji wa Ukiriguru - Usagara ambayo ilitembelewa na Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza tarehe 23,Mei,2024 ambapo Kamati ilijionea hatua ya miradi hiyo na kuwataka kukamilisha miradi kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.