Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na kutoridhishwa na baadhi ya miradi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe, Antony Diallo pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wameonyesha kutoridhishwa na utekelezaji na usimamizi wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Kata na vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambapo kwa mwonekano na maelezo ya Wataalam inaonyesha kutotekelezwa na kusimamiwa kikamilifu na kutozingatia ubora wa majengo ya Serikali.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe, Antony Diallo amesema kwa ujumla baadhi ya miradi haikutekelezwa na kusimamiwa ipasavyo hususan Jengo la Mabaara katika Sekondari ya J.Magufulu Kata ya Gulumungu ambalo Serikali imetoa shilingi Milioni 90 kukamilisha ujenzi amabo unaonekana kutokamilika vizuri kutokana na fedha kutumika zote na bado ukamilishaji unaendelea.
Mhe, Diallo aliongeza kwamba kuna ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Mwamaguha ambapo zilitolewa shilingi Milioni 50 kukamilisha Jengo lakini ujenzi haukusimamiwa vizuri na Wahandisi wa Halmashauri na Kamati ya ujenzi kutoshirikishwa katika hatua zote za ujenzi, ikizingatiwa kwamba Serikali kwa sasa inasimamia na kutekeleza ujenzi kwa kutumia Force Akaunti kwa matumizi ya mafundi wa maeneo husika na manunuzi ya vifaa kwa bei ya sokoni.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ameeleza kuwa Kamati imekagua na kubaini mapungufu na taarifa itaandaliwa vizuri na kuwasilishwa katika vikao vya chama Mkoa pamoja na kuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo yenye jumla ya Kata 27 kufuatilia na kushughulikia mapungufu yaliyobainika na baada ya hapo hatua za kiutumishi zitaanza kuchukuliwa kwa watakaohusika katika ubadhilifu ama uzembe katika utekelezaji wa miradi husika..
Mhandisi Robert Gabriel amesema kwamba usimamizi wa matumizi ya fedha za umma unaonekana kutozingatia kanuni na taratibu na Watendaji wameonekana kutokuwa waadilifu katika matumizi ya fedha na mali za umma, ametolea mfano Serikali imetoa fedha shilingi Milioni 90 kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya Maabara katika Sekondari ya J. Magufuli ambapo ujenzi umefanyika na fedha yote imetumika na hakuna bakaa ya fedha na Jengo linaelekea kutokamilika vizuri wakati huo Serikali imetoa fedha shilingi Milioni 60 ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu kwa ramani ile ile katika Sekondari ya Sanjo na Jengo limekamilika vizuri na kwa ubora na limeanza kutumika .
Katika ziara hiyo ya Kamati ya Siasa Mkoa ambayo iliambatana na Wajumbe wote , Wataalamu wa Sekretarieti ya Mkoa, Waataalam wa Wakala wa Serikali, RUWASA, TARURA, TANNESCO, pamoja na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Misungwi, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Misungwi, Wakuu wa Idara na VItengo wa Halmashauri wameweza kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo utekelezaji wa za shughuli za miradi ya Ujenzi wa Maabara katika Sekondari ya J. Magufuli, Ukamilishaji wa Jengo la Zahanati ya Mwamaguha, ukamilishaji wa ujenzi wa Jengo la Zahati ya Mhungwe, Mradi wa ununuzi wa Dawa na vifaa Tiba katika Haospitali mpya Wilaya ya Misungwi, Jengo la ofisi za Halmashauri, Jengo la Soko la Kijiji cha Kigongo na Mradi wa utoaji Fidia katika Eneo la Standi ya Mabasi Nyashishi.
Jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi lilojengwana Mkandarsai Wakala wa Mjaengo Tanzania (TBA) kwa gaharama ya shilingi Biliioni 2.8 limekamilika na Watumishi wameshahamia na kuanza kazi, Kamati ya Siasa Mkoa imepongeza juhudi na usimamizi wa Wtendaji na Viongozi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe, Antony Diallo (kulia) akizungumza na Mhe Diwani wa Kata ya Kijima Ezekiel Kanzaga na Viongozi wengine kuhusu hatua za ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Mwamaguha lilivyojengwa kwa mafundi wenyeji na manunuzi ya vifaa (Katikati ni) Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel akisikiliza mjadala huo. katika ziara ya Kamati ya Siasa kukagua ujenzi wa Zahanati hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.