Kamati ya Lishe yafanya kikao cha robo ya kwanza cha mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajilli ya kupitia na kujadili taarifa mbalimbali za maendeleo ya hali ya Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuishia mwezi Septemba 2024.
Akizungumza mapema katika kikao hicho leo tarehe 15 Novemba2024 Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi amewataka Wajumbe ambao ni baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kuendelea na ufuatiliaji na usimamizi wa hali ya Lishe katika maeneo yao na kujiandaa kutenga Bajeti ya shughuli za Lishe katika Mpango na Bajeti ya mwaka ujao 2025/2026 ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli za Lishe kuimarika zaidi.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi. Lucia Bazili wakati akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya hali ya Lishe Wilayani Misungwi ameeleza kwamba hali ya utoaji wa Lishe katika shule za msingi na Sekondari imeimarika kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 na watoto wanaendela kupata angalau mlo mmoja wakati wa masomo na Wazazi na Wananchi wamehamasika katika suala la uchangiaji wa Chakula mashuleni, amewaomba Watendaji na Wataalam wa Halmashauri kuendelea kufuatilia na kusimamia utekelezaji shughuli za Lishe ili kuweza kufikia malengo ya Mkataba wa Lishe.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Dkt. Clement Morabu amesema kuwa lengo la kikao cha Kamati ya Lishe ni kukumbushana na kujadili kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa mikakati ya lishe katika Halmashauri , pamoja na kuwakumbusha wajumbe kuhusu majukumu yao na viashiria vya Mkataba wa lishe.
Katika kikao hicho cha Kamati ya Lishe kimehudhuriwa na Wakuu wa Idara na Wataalam mbalimbali kutoka sekta za afya, elimu, kilimo, na maendeleo ya jamii, Fedha, Mipango na Ufuatiliaji, Habari na Mawasiliano pamoja na Utawala
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.