Kamati ya Huduma za Kijamii yaridhishwa na kufurahishwa na utekelezaji wa ujenzi na Ukarabati wa Miradi ya Sekta ya Elimu katika Shule za Msingi za Busagara,Kigongo na Mitindo pamoja na Shule ya Sekondari Idetemya na kupongeza juhudi zinazofanywa kwa usimamizi wa Kamati za Shule.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe,Ngwanza Nyahehe alieleza kuhusu Miradi iliyotembelewa ambayo ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la Vijana katika Hospitali ya Misungwi kwa Shillingi 15,420,00/=, Ujenzi na Ukarabati wa Bweni,Jiko na Vyumba 4 na ofisi 1 shule ya Msingi Mitindo,Mradi wa Ujenzi wa Maji Bomba wa Nyahiti-Misungwi kwa shilingi 9,000,000,000/= na Ujenzi wa Choo matundu 7 na utengenezaji wa thamani za shule katika Shule ya Msingi ya Busagara kwa shillingi 9,933,145/=,Mradi wa ukarabati wa Vyumba 14 vya Madarasa na ujenzi wa Mfumo wa Kuvuna Maji katika Shule ya Sekondari Idetemya kwa Shilingi 63,000,000/= pamoja na Ukabarabati wa Vyumba 8 na utengenezaji wa thamani kwa shilingi 9,934,120/= na Ujenzi wa Choo Matundu 16 kwa gharama ya shilingi 30.000.000/=
Mwenyekiti huyo wa Kamati alisema kwa ujumla Miradi hiyo imetekelezwa kwa kiwango na thamani ya fedha imeonekana na kueleza kuwa Kanmati za Shule zimesimamia kikamilifu na kuzingatia ushauri wa Wataalam wa Idara ya Ujenzi pamoja kuzingatia hatua za manunuzi .
Pichani juu ni Jengo la Choo cha Wavulana matundu 7 kilichokamilika kwa Shillingi 6,313,145 katika Shule ya Msingi Busagara
Picha ikionyesha Ujenzi wa taki lenye Ujazo wa lita 70,000 la kuvuna Maji lililojengwa katika Shule ya Sekondari Idetemya.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.