Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango imeiagiza Menejimenti ya Halmashauri kuhakikisha inasimamia kikamilifu Miradi ya Maji inayotekelezwa na kukamilika kwa wakati.ili kuleta manufaa kwa Wananchi wa Wilaya ya Misungwi kwa kupata huduma bora ya Maji.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe,Antony Bahebe Masele alieleza hayo wakati wa Ziara ya Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maji ya Ihelele- Mbarika na Mradi wa Ngaya -Mbarika ambao umeshaanza na unaendelea katika hatua ya kujenga Matanki mawili ambapo amewataka Wataalam kuhakikisha wanasimamia Wakandarasi na kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye hatua zote za utekelezaji Miradi husika ili iweze kukamilika kwa kiwango na ubora zaidi.
Pichani ni Tanki la Maji lenye ujazo wa Mita 45,000 linaloendelea kujengwa katika Kijiji cha Lutalutale
Kamati hiyo ilifanya Ziara kwa ajili ya kukagua na kuona shughuli zilzotekelezwa kwa kipindi cha robo ya pili kinachoishia mwezi Disemba 2018 ambapo wameweza kutembelea Miradi ya Maji katika Kata ya Mbarika na Ilujamate na kutoa ushauri na mapendekezo kwa Menejimenti
Wajumbe wa Kamati hiyo walipata fursa ya kuona hali halisi ya utekelezaji wa Miradi husika kwa kukagua kwenye chanzo cha Maji cha Ihelele pamoja na Matanki ya Nyangh'omango ambacho kitasambaza Maji katika Kijiji cha Nyang'homango ,na kuona hatua za Ujenzi wa Machoteo 9 yaliyokamilika kutoka Kijiji cha Ngaya,Bugisha,na Lutalutale na tanki lenye ujazo wa lita 45,000 linaloendelea kujengwa katika Kijiji cha Lutalutale.
Kwa upande wake Mhandisi wa Maji wa Halmashauri, Ali Mruma alieleza na kufafanua kuhusu utekelezaji wa Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya CMG COMPANY LTD kwa kujenga Matanki mawili,Kutandaza mabomba kutoka Ngaya hadi Mbarika na kujenga Machoteo 9 kwa ajili ya Matumizi ya Wananchi na Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2018.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango wakikagua Mojawapo ya Machoteo ya Maji yaliyojengwa kwenye Mradi wa Ngaya-Mbarika.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.