Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango yaridhishwa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa vizuri na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe, Kashinje Machibya amepongeza Menejimenti na Watendaji kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali, wafadhili na michango ya Wananchi.
Mhe, Machibya amesema kwamba kiujumla miradi imetekelezwa kwa kiwango na ubora na thamani ya fedha inaonekana ambapo katika mradi wa ujenzi wa Zahati ya Mwawile iliyopo Kata ya Nhundulu ambayo imetengewa kiasi cha shilingi milioni 400,000,000/= fedha ya UVIKO 19 ikiwa na majengo mawili,Jengo ni Jengo la wagonjwa wanje (OPD), Jengo la maabara.
Aidha Mhe, Machibwa amewataka wahandisi wanaosimamia ujenzi wa Zahanati hiyo kuzingatia vigezo na ushauri vilivyowekwa na kitaalamu na siyo vinginevyo,Sambamba na hilo amesema sehemu zinazohitaji marekibisho zifanyike kwa wakati kuondoa gharama zisizo za lazima.
Mhe, Kashinje Machibya amesema kwa ujenzia unaendelea katika Shule ya Sekondari Mwanangwa iko katika hatua nzuri na inaridhisha na kuwataka wasimamizi wa Shule hiyo waendelee kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maelekezo wanayopewa na wataalamu ili kufanya kazi nzuri na yenye viwango bora vinavyotakiwa katika ujenzi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi Bw,Benson Mihayo amesema kwa kushirikiana na Menejimenti ataendelea kusimamia kwa uadilifu mkubwa na kuhakikisha miradi maendeleo yote inakamilika ili wananchi waweze kupata huduma bora inayostahili kwa wakati.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya Bw,Clement Morabu ametoa shukrani za pekee kwa Serikali ya awamu sita kwa kajiri watumishi katika Zahati hiyo,na tayari wapo kituoni wanachapa kazi,hata hivyo amsema kuna nyumba ya watumishi ambayo imegharimu milioni 90,000,000/=kwa kutumia force akaunti,ambapo ujenzi unaendelea na fedha bado inahitajika ili kumalizia vitu vilivyo baki ikiwemo umaliziaji wa vyoo katika nyumba hiyo.
Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Kashijnje Machibya wa pili kutoka mkono wa kulia akipata taarifa ya mradi wa Zahanati ya Mwawile iliyo Kata ya Nhundulu ambapo aliongazana na wajumbe wa kamati ya fedha na mipango katika Ziara ya ukaguzi.Kushoto ni Dkt Clement Morabu akitoa maelezo juu ya mradi huo.
Baadhi ya Waheshiwa Madiwani wakiongozwa na Mhe,Kashinje Machibya wa pili kutoka (kushoto),wa pili kutoka kulia ni Mhe,Mganyizi Ferouz diwani wa kata ya Misungwi wakiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa mradi wa Zahanati Mwawile kata ya Nhundulu .
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Fedha Uongozi na mipango kushoto ni Mhandisi Wiliam,(katikati) Afisa utumishi Yusuf Lubuga wakitembelea Mradi wa Zahanati ya Mwawile ambapo walikagua na kutoa ushauri juu ya mradi huo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.