Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkaoani Mwanza yaridhishwa na Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na kusimamiwa na Menejimenti kwa kutumia Mapato ya ndani pamoja na mapato kutoka Serikali kuu.
Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya kipindi cha robo ya kwanza kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 mwezi Julai –Septemba ambapo imekagua mradi wa ujenzi wa matundu ya vyoo 24 katika shule ya Msingi Buganda,Ujenzi wa Manawa Sekondari,Ujenzi wa mradi shule ya sekondari Mwanangwa,Mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi,Mradi wa kituo cha Afya Usagara,Mradi wa kituo cha Afya Fela na Mradi wa kituo cha Afya Koromije.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe, Kashinje Machibya amepongeza Menejimenti na Watendaji kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali, wafadhili na michango ya Wananchi.
Mhe, Machibya amesema kwamba kiujumla miradi imetekelezwa kwa kiwango na ubora na thamani ya fedha inaonekana ambapo katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi iliyopo Kata ya Misungwi ipo katika hatua ya kuridhisha ambapo majengo manne yapo katika hatua ya ukamilishwaji ambalo ni jengo la Upasuaji,jengo la Upasuji la Wanaume na Wanawake pamoja na jengo la Mochwari.
Aidha Mhe, Machibwa amesema mradi wa ujenzi huo utakamilika mwishoni wa Mwezi wa 11,2022 Mwaka huu na kuwataka wahandisi wanaosimamia ujenzi wa Hospital hiyo kuzingatia vigezo na ushauri vilivyowekwa na kitaalamu na siyo vinginevyo na kuwataka kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa weledi.
Bw,Machibya amesema Ujenzi wa majengo hayo utakapokamilika utasidia Wananchi kupata huduma ya Upasuaji kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa pindi watakapofika Hospitalini hapo kupata huduma hiyo.
Mhe, Machibya amesema kwa ujenzia unaendelea katika Shule ya Sekondari Manawa uko katika hatua nzuri na inaridhisha na ametoa rai kwa watendaji kuongeza kasi ya ukamilishaji wa vyumba 4 vya madarasa katika shule hiyo ili kufikia Januari 2023 wanafunzi waanze masomo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi Mhe,Joel Dogani diwani wa Mbarika alimtaka muwekezaji aliyenunua mlima kwa shilingi milioni 80 eneo la zahanati ya fela iliyopo kata ya Fela kuleta nyaraka za mkataba kwa mkurugenzi na kujiridhisha na kuona kama ilizingatia kanuni na utaratibu .
Katika ziara hiyo Wajumbe wa Kamati kupitia Mwenyekiti wao wamempongeza mkurugenzi wa Halimashauri ya Wiaya ya Misungwi kwa namna anavyoshiriki kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi Bw,Benson Mihayo amepokea pongezi hizo na ameziomba Kamati hizo zinazosimamia miradi kuwa makini na matumizi ya fedha na Serikali kutekeleza shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya Bw,Clement Morabu ametoa shukrani za pekee kwa Serikali ya awamu sita kwa kuleta mashine ya Upasuaji katika Hospitali hiyo,ambapo amsema pindi itakapoanza kutumika itahudumia Wananchi kwa kiwango kikubwa na itarahisisha kuwasogezea huduma kwa ukaribu Zaidi.
Ziara ya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya robo ya mwaka wa fedha hufanyika kila baada ya robo ya kwanza kukamilika Julai hadi Septemba mwaka 2022/2023 na hii ni ziara ya robo ya kwanza ikiwa lengo kukagua, kushauri na kubaini changamoto na kuzitafutia suluhisho.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango wakiendelea na ziara ya ukaguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi ili kubaini changamoto na kuzitafutia ufumbuzi .
Baadhi ya Wajumbe wakiwa kwenye ziara ya kukugua miradi mbalimbali ya Maendeleo,wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya akitoa maelekezo kwa wataalamu katika mradi wa ujenzi wa Sekondari Mwanangwa leo mapema.
Moja ya mashine ya kisasa Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi ambapo Mradi huo pindi utakapokamilika mashine itasaidia kutoa huduma kwa Wananchi wa Wilaya ya Misungwi pamoja na maeneo ya jirani.
Mwonekano wa Majengo ya vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Manawa iliyopo Kata ya Misasi ambapo yapo katika hatua ya ukamilishwaji,Shule hiyo inataraji kupokea Wanafunzi Januari 2023.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.