Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yapongeza Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na kusimamiwa na Menejimenti kwa kutumia Mapato ya ndani pamoja na mapato kutoka Serikali kuu.
Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango imefanya ziara tarehe19,Februari,2024 ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Mwambola,Ujenzi wa Sekondari Mwanangwa pamoja ujenzi vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Mwanangwa na ujenzi wa matundu 6 ya vyoo katika shule hiyo.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe, Kashinje Machibya amepongeza Menejimenti na Watendaji kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali, wafadhili na michango ya Wananchi.
Mhe, Machibya amesema kwamba kiujumla miradi imetekelezwa kwa kiwango na ubora na thamani ya fedha inaonekana ambapo katika mradi wa ujenzi wa Shule ya sekondari Mwambola iliyopo Kata ya Misungwi ambayo imegharimu zaidi ya fedha Shilingi Milioni 500.
Aidha Mhe, Machibwa amesisisitiza wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule hiyo kwamba miradi yote inayotekelezwa na Serikali ni jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Jambo pekee ambalo mnaweza kumlipa ninyi ni kufaulu vizuri,amewaleteni shule walimu wazuri na uongozi ambao upo karibu na ninyi,jukumu lenu kama Watoto ni kufaulu vizuri”.
Mhe, Machibya amesema kuwa mradi wa ujenzi wa vibanda unaendelea katika stand ya Misungwi ambao uko katika hatua ya upauji,Ofisi ya Mkurugenzi ipitie upya fedha iliyoidhinishwa kujenga vibanda hivyo ili kujiridhisha kama inaendana thamani ya ujenzi wa mradi huo.
Katika ziara hiyo Wajumbe wa Kamati kupitia Mwenyekiti wao wamempongeza Mkurugenzi pamoja na timu Menementi kwa namna anavyoshiriki kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru amesema kwa kushirikiana na Menejimenti ataendelea kusimamia kwa uadilifu mkubwa na kuhakikisha miradi maendeleo yote inakamilika ili wananchi wa Misungwi waweze kupata huduma bora inayostahili kwa wakati.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe.Kashinje Machibya Kushoto,wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Joseph Mafuru (katikati) ni Afisa Elimu Sekondari Bi. Diana Kuboja akipokea taarifa fupi ya ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Mwambola hapo jana.
Mwonekano wa baadhi ya majengo wa ya Shule ya Sekondari Mwambola iliyopo Kata ya Misungwi kijiji cha Mwambola ambapo imegharimu kiasi cha fedha zaidi ya Shilingi Milioni 500.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.