Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango imeagiza Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuhakikisha Miradi iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2017/2018 kuanza kufanya kazi iliyokusudiwa ili kunufaisha Wananchi pamoja na kuongeza Mapato ya Halmashauri.
Akizungumza kuhusu Utekelezaji wa Miradi hiyo wakati wa Ziara Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe,Antony Masele Bahebe aliwataka Watendaji wa Halmashauri kukamilisha Miradi haraka na kuanza kutumika ili kutoa huduma kwa Walengwa pamoja na kunufaisha Halmashauri.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa Stendi ya Mabasi Madogo (Hiace) Nyashishi kwa Tsh,10,000.000/= ,Ujenzi wa Stendi ya Mabasi Madogo na Choo Usagara kwa gharama ya Tsh,10,000,000/= na Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Fella kwa Tsh,44,000,000/= na Ujenzi wa Machinjio ya Usagara kwaTsh,10,000,000/= pamoja na Mradi wa Maji wa Nyahiti Misungwi kwa Tsh,9,000,000,000/= ambapo Kaamati iliridhishwa na baadhi ya ujenzi wa Miradi na kuwataka ikamilike kwa wakati na kwa kiwango.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.