Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yakemea vikali baadhi tabia ya Watumishi wanaopokea na kutoa rushwa katika utoaji wa huduma ya Afya Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango imefanya ziara tarehe 08,Mei,2024 ya kutembelea na kukagua utoaji wa huduma bora kwa wananchi katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi,Vituo vya Afya vya Usagara,Misasi,Koromije,Mbarika,Busongo,pamoja na baadhi ya Zahati ili kujionea hali halisi namna wananchi wanavyopata huduma bora na kwa wakati pamoja na kuongea na watumishi katika vituo hivyo.
Akizungumza katika ziara hiyo katika Kituo cha Afya Mbarika, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe, Kashinje Machibya amesema jukumu la watumishi wa umma ni kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa kuwahudumia kwa lugha ya staha na kuwajali pasipo kubagua mtu yeyote pindi anapohitaji huduma katika Hospitali,Vituo vya afya pamoja na Zahati kwa kuzingatia miiko na kanuni na misingi ya kazi katika kuwahudumia wagonjwa.
Aidha Mhe, Machibya amesema kwamba kuna baadhi ya Vituo vya afya havitoi huduma kama inavyotakiwa na kuwasababishia wagonjwa adha ya Kwenda kutafuta huduma sehemu nyingine,pamoja na kuwatoza baadhi ya wagonjwa fedha kwa ajili ya kupata matibabu ikiwemo huduma ya Mama wakati wa kujifungua amesisitiza suala hilo halikubaliki.
Katika hatua nyingine Mhe, Machibwa amekea vikali baadhi ya tabia za watumishi kuondoka kwenye vituo vya kazi kabla ya muda wa kazi kuisha ikiwa pamoja wizi wa dawa za Serikali,na kutoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao wanakiuka maadili ya kazi wawapo kazini na iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizo.
Katika ziara hiyo Wajumbe wa Kamati kupitia Mwenyekiti wao wamesema wataendelea kutembelea na kukagua utoaji wa huduma bora kwa wananchi katika Wilaya ya Misungwi,na kutoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na utu pindi wanapowahudumia wagonjwa.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi Bw.Steven Singira amesema kwa kushirikiana na Menejimenti ataendelea kusimamia nidhamu za watumishi na kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kutoa huduma bora na kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.