Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.9 zinatazowanufaisha Wanafunzi kupata elimu Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miradi iliofanyika 21 Oktoba 2024, Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Mhe, Kashinje Machibya amepongeza Menejimenti kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali, Shule ya Msingi Mabuki inayojengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 351.5 pamoja na na shule ya sekondari Amali yenye gharama ya Shilingi Bilioni 1.6.
Katika hatua nyingine Mhe, Machibya amewataka Watendaji wa Mradi hiyo kuhakikisha wanazingatia manunuzi kwa wakati kupitia mfumo wa NEST ili kuepuka kupata changamoto za ucheleweshwaji wa Miradi hiyo pia amewataka watoa risiti katika vituo kuhakikisha wanazingatia utendaji wa kazi ikiwa ni kutoa risiti kwa wakati kwa madereva ili kuimarisha upatikanaji wa mapato ya ndani ya Halmashari ambapo zitakua chanzo cha maendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Misungwi .
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi Bw.Addo Missama amesema kwa kushirikiana na Menejimenti atasimamia kwa uadilifu mkubwa na kuhakikisha miradi maendeleo yote inakamilika ili wananchi wa Misungwi waweze kupata huduma bora inayostahili kwa wakati.
Kwa upamde wake Mhandisi ujenzi Wilaya ya Misungwi Bw, Edmund Kasiga amesema kuwa Shilingi Bilioni 1.6 itatumika kujenga shule ya Sekondari Amali yenye Madarasa 4 na ofisi 1, Jengo la Utawala , maabala 2 ,maktaba, nyumba ya mwalimu .chumba cha TEHAMA ,mabweni, vyoo 4 Wavulana na 4 Wasichana ,tankila maji la ardhini ,uwekaji vifaa vya umeme,karana ufundi uashi , uwamja wa mpira wa nyavu na uwanja wa mpira wa mikono.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mabuki Bi. Peruzi Chacha ameeleza kuwa gharama ya Shilingi Milioni 351.5 itatumika kujenga Shule ya Msingi Mabuki yenye Madarasa 2 ya awali , madarasa 7 , jengo la utawala na vyoo 14 kwa wabulana na wasichana ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Disemba 19 , 2024.
Katika ziara hiyo miradi iliyokaguliwa ni shule mpya ya msingi Mabuki, , pamoja na shule ya sekondari amali, na kutembela vituo vya kutoa risiti ikiwemo Kona ya Mitindo , Stendi ya Misungwj stend ya nyashishi , kituo cha Sanjo pamoja na kituo cha ukaguzi Usagara.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.